Featured
Loading...

Sentensi za Profesa Tibaijuka alivyosimama bungeni kuchangia bajeti ya Viwanda na Biashara



Mei 6 2016 ilikuwa ni zamu ya  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwasilisha Bungeni Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Baada ya uwasilishaji huo Wabunge walipata nafasi ya kuchangia maoni yao kuhusu bajeti hiyo, hapa nakukutanisha na Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka alivyosimama na kutoa mchango wake..
>>’Mimi ninafahamu kama Mwanauchumi ni lazima viwanda vinaendana na kilimo, huwezi kuendeleza viwanda kama hujaendeleza kilimo. Ni lazima tuwe na malighafi kwamfano mazao ya mchele na alizeti
Mimi kama mchumi ntasema kwamba Taifa hili halina sababu yoyote isipokuwa katika hali ya dharura kukubali kuagiza sukari, mchele au alizeti kutoka nje, lazima kuwe na mkakati wa kulinda viwanda
Hali hiyo tujipange sasa, tulio wengi ni wakulima, wavuvi na wafugaji. Sasa mnatuwezeshaje? ninaposema sukari isiingie, ikiingia itaua viwanda vya sukari.. hata mtoto wa shule anajua hilo, lazima Wizara iwe na utaratibu wa kuingiza sukari lakini sio kutumia wafanyabiashara

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top