Featured
Loading...

Chadema Waamua Kuwaacha CCM Wafanye Mkutano wao Dodoma...Wao Kufanyika Dar



Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limehamishia mkutano wake wa kamati ya utendaji jijini Dar es Salaam na kuuondoa mjini Dodoma ulikopangwa kufanyika.

Awali, Bavicha ilikuwa imehamasisha vijana wa chama hicho kwenda Dodoma kwa wingi kwa ajili ya “kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa”.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe aliwazuia vijana hao, lakini Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema wiki iliyopita kuwa wameandaa mkutano wa Kamati ya Utendaji wa Baraza hilo leo mjini Dodoma na ungefunguliwa na Mbowe.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top