Elvan Stambuli, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein
ameutabiria uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajia kufanyika kesho
visiwani humo.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum ofisini kwake Dar
juzi, Maalim Hassan alisema uchaguzi huo utafanyika kwa amani na wala
hakutakuwa na fujo.
“Uchaguzi utapita salama na mshindi atapatikana, kinyota inaonesha hakutakuwa na purukushani zitakazotokea wakati wa uchaguzi huo,” alisema.
“Uchaguzi utapita salama na mshindi atapatikana, kinyota inaonesha hakutakuwa na purukushani zitakazotokea wakati wa uchaguzi huo,” alisema.
Aliongeza kuwa, wananchi hawapaswi kuwa na hofu kwani hakuna ukiukwaji
wa taratibu na uvunjifu wa amani utakaofanyika siku hiyo ya uchaguzi.
Hivi karibuni kumekuwa na hofu visiwani humo kutokana na matukio
yanayohusishwa na siasa ambapo nyumba kadhaa zilichomwa moto kisiwani
Pemba na nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame
ililipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu wasiojulikana
saa 5.00 usiku huko Kijichi, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Uchaguzi wa Zanzibar unatarajiwa kurudiwa kesho baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha kwa madai kuwa ulikuwa na kasoro nyingi

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )