Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini limelalamikiwa kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa msukumo wa binafsi ya baadhi ya watumishi wa baraza hilo na kwamba, sababu zilizotolewa ni za ‘kipuuzi’.
Pia imeleezwa kwamba, hatua hiyo ni juhudi za kurudisha nyuma ama kukwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa Tiba Asili.
Hayo yamesemwa leo na Mohamed Matokeo, Mwenyekiti wa Baraza la Waganga wa Tiba, Ushauri na Utafiti wa Dawa Asili Tanzania (Bawata) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
“Bawata tukiwa chombo huru cha waganga wa tiba asili, tunasikitika sana utendaji kazi unaofanywa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambacho ni chombo cha kiserikali kilichopewa mamlaka ya kusimamia taaluma hii na kuiendeleza,” amesema na kuongeza;
“Lakini baraza hilo limekuwa ni chombo kinachorudisha nyuma fani ya tiba asili hapa nchini, kwani limekuwa likikwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa tiba asili walioonesha ufanisi katika kutoa huduma ya tiba asili.
Imekuwa kawaida kwa baraza hilo kuitisha au kuwafungia waganga wa tiba asili na vituo vyao kwa sababu zinazoonekana ni za kibinafsi.”
Matokeo ametoa mfano wa tukio lililotokea jana la kufungwa kwa baadhi ya vituo vya tiba asili ambapo amesema kuwa, wahusika walifungiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea na au kuhojiwa.
“Sisi bawata tunapinga hatua hii ya kiuonevu kwani wametoa maamuzi ya kuwafungia bila ya kuwahoji wahusika, tena hawa ni waganga halali kisheria wamesajiliwa na wanalipa kodi vizuri,” amesema.
Sharifu Karama, Katibu Mkuu Taifa wa Bawata amedai kuwa, kuna baadhi ya watumishi wa afya wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba asili kwamba ndiyo wanaochochea kukandamizwa kwa masilahi ya waganga wa tiba asili nchini.
“Kuna baadhi ya watumishi wa afya wanauza dawa za tiba asili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwenye jengo la serikali.
“Kutokana na hali hiyo, Bawata tunaamini kwamba, baraza la tiba asili na tiba mbadala linaongozwa na waganga wa kisasa na kwamba tuna taarifa kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa baraza hilo nao wanauza dawa asili kwa hiyo wanalitumia baraza kutimiza hadhma yao,” amesema.
Hata hivyo, Foreplan ilianza kuwindwa na Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Afya baada ya kufanya ziara ya kushtukiza tarehe 15 Desemba mwaka jana na kuibua maswali mengi.
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutolewa siku saba za uchunguzi na kwamba, kinachofanyika sasa kinatajwa kuwa ni matokeo ya ‘dhamira’ iliyooneshwa baada ya ziara hiyo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )