Featured
Loading...

Wasanii Wakongwe Wa Bongo Fleva walivyopagawisha Mkesha Wa Pasaka, Dar


IMG_5641Staa mkongwe kunako Bongo Fleva, Prince Dully Sykes akikamua jukwaani.
IMG_5663
Sir Juma Nature naye alikuwepo jukwaani kukinukisha.
IMG_5679
Staa mkongwe kutoka Wateule, Jaffarai naye alikuwepo kuzikonga nyoyo za mashabiki.
IMG_5688Afande Sele ‘Baba Tunda’ akiwapigia saluti mashabiki mara baada ya kukamua Wimbo wa Mtazamo.
IMG_5699
Inspector Haroun ‘Babu’ akikamua Wimbo wa Mtoto wa Geti Kali.
IMG_5732
Mmoja wa wasanii wakongwe akikamua jukwaani.
IMG_5771
Kundi linalotikisa tangu kitambo la Mabaga Fresh likikamua jukwaani.
IMG_5804Mkali Soggy Dog Hunter naye alikuwepo kumpa tafu Promota Bonga.
IMG_5868
Mkali wa nyimbo za Uswahilini, Suma G akikamua jukwaani.
IMG_5892
Staa kutoka kundi maarufu la Daz Nundaz, Ferooz akikamua kwa hisia jukwaani.
IMG_5664
Ilikuwa burudani! Staa mkongwe, Sister P akifuatilia jambo kwa makini.
IMG_5705
Kama karambwanda! Nature haokuona aibu baada ya kukata keki ya Promota Bonga kiisha kujisevia.
IMG_5697Nature akiwa katika picha ya pamoja na Mabaga Fresh pamoja na Sister P.
IMG_5635
Mashabiki waliotimba katika shoo hiyo wakishangweka.
AMA kweli! Ng’ombe hazeeki maini, hivyo ndivyo walivyodhihirisha wasanii wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva mara baada ya kuporomosha bonge la shoo katika Mkesha wa Sikukuu ya Pasaka.
Mkesha huo ulifanyika jana usiku,  katika Ufukwe wa Sunrise uliopo Kigamboni jijini Dar uliendana na sherehe ya kutimiza miaka 25 ya promota maarufu nchini,  Majid Mdoe ‘Promota Bonga’ . Huku wasaniii kama Afande Sele, Dully Sykes, Jaffarai, Suma G, Manzese Crew, Mabaga Fresh,  Zig Zag Crew, Fanani wa Hard Blastaz Crew, Soggy Dog, Inspectour Haruni ‘Babu’ Juma Nature, Sister P, Sold Ground Family Feruzi, Rich One na wengine kibao wakiwakumbusha mashabiki wao kwa muziki uliowahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma.
Shoo hiyo iliandaliwa na  na mmoja wa mapromota wakongwe wa muziki huo, Promota Bonga akishirikiana na Kituo cha Redio cha Times FM kilichopo Kawe jijini Dar.
IMG_5643
IMG_5645
IMG_5659
IMG_5718
IMG_5719
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top