Featured
Loading...

Donald Trump Amsifu Saddam Hussein na Gaddafi...Adai Dunia Ingekuwa na Amani Kama Wangekuwepo


Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.

Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North
Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.
“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.”
Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni
ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.

Saddam Hussein aliongoza Iraq kuanzia 1979 hadi 2003
Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”

Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top