MKE wa rapa maarufu Kanye West kutoka Marekani, Kim Kardashian
amemuonesha mtoto wao Saint West kwa mara ya kwanza mbele ya umati.
Kim amemwonesha mwanaye huyo wa pili mwenye umri wa miezi saba wakati wa
kipindi cha Keeping Up With The Kardashians kinachoruka kwenye runika
kikielezea maisha halisi ya Kim Kardashian na familia yake.