Featured
Loading...

JB kufungua mwaka na filamu ‘Kalambati Lobo’ baada ya kukaa kimya toka mwaka uanze

Kampuni ya Jerusalem Films inayomilikiwa na msanii wa filamu Jacob Stephen ‘JB’ baada ya kufanya poa na filamu yake ‘Chungu Cha Tatu’ iliyoachiwa mwisho wa mwaka jana, inajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Kalambati Lobo’.
13726745_1136528649741779_6241745022786990933_n
Filamu hiyo ambayo inaingia sokoni mwezi August mwaka huu, imewakutanisha tena wahusika wa filamu ya Danija, JB pamojana Diana Kinaro.
“Wapenzi wa Jerusalem Films, napenda kuwajulisha kuwa movie yetu ya Kalambati Lobo itakuwa madukani mwezi August,” aliandika JB kupitia instagram.
Aliongeza, “Najua tangu mwaka huu uanze tumekuwa kimya lakini ni kwa sababu ya ratiba ya kutengeneza kazi zingine kutoka Jerusalem Films baada ya Chungu Cha Tatu, safari hii namleta kwenu Diana Kimaro, hii ni zaidi ya Danija, kaa tayari, Kalambati Lobo nikiwa na Diana Kimaro,”
Jerusalem Films ni moja katik ya kampuni za filamu ambazo zinafanya vizuri nchini kutokana na filamu zake nyingi kufanya vizuri sokoni.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top