Featured
Loading...

Samatta kaifungia tena KRC Genk Ligi Kuu Ubelgiji leo July 31


July 31 klabu ya KRC Genk ambayo inachezewa na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta, bado inajiandaa na mchezo wa pili wa round ya pili wa kuwania kufuzu hatua ya Makundi ya Europa League dhidi ya Cork City ya Ireland, July 31 kabla ya mchezo huo imecheza mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KV Oostende.
Mchezo huo ambao ndio mchezo wa kwanza kwa Mbwana Samatta kupata nafasi ya kucheza akiwa na KRC Genk katika mchezo wa mwanzo wa msimu, KRC Genk wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ambayo yamefungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 50 na  Mbwana Samatta aliyeingia akitokea benchi dakika ya 93.
Mbwana Samatta wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Cristal Arena aliingia dakika ya 80 alitokea benchi, kwani inaonekana kocha wa KRC Genk kuwaanzishia benchi baadhi ya wachezaji wake tegemeo kutokana na kukwepa majeruhi ili asije kuwakosa katika mchezo wa marudiano Europa League dhidi ya Cork City August 4 Ireland.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top