

Ndugu zangu,
Picha
hizo zinajieleza zenyewe. Hakika inapendeza kuona Watanzania kwa desturi
zetu ni watu wenye kujumuika pamoja bila kutanguliza tofauti za
kisiasa. Ndio maana ya kusema, kuwa hili la maandamano ya UKUTA ni balaa
tunalojitakia huku waandaaji wakijua fika hivyo.
Tukumbuke,
kwa mwanadamu, siku zote, chuki hupandikizizwa, chuki humeea na chuki
huzaa chuki. Kamwe, mavuno ya chuki hayajapata kuwa ya heri.
Ni jambo
la hatari kwa nchi, pale kikundi kidogo cha watu kinapoachwa kifanye
mzaha na hata ushabiki kwa jambo lenye kupelekea maafa kwa wengi. Lililo
bora ni kwa watu hao kuonywa mapema kuacha kufanya mzaha na ushabiki
huo.
Maggid,
Zanzibar.(P.T)
Tuma Maoni
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )