Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA
Madam Mery akaniwahi kunishika shati na kuanza kuniomba niache
vurugu,mkuu wa shule akanyanyuka kwa hasira na kunisogelea na kunizaba
kofi lililopelekea nikazidi kupadwa na hasira,Madam Mery akaendelea
kuning’ang’ania kwa nguvu zake zote ila kutokana na nguvu nilizo nazo
nikajitoa mikononi mwa madam Mery na kumfwata mkuu wa shule na kuanza
kumrushia ngumi zisizo na idadi na uzuri zaidi kipindi nipo mdogo baba
yangu alikuwa akinifundisha mbinu za kuweza kupigana kiasi kwamba hadi
ninakua mkubwa swala zima la kupigana kwangu ni lakawaida.Waalimu wa
kiume waliopo eneo la shule wakaja kutuzuia japo kuwa mkuu wa shule ni
mzee kidogo ila na yeye alijitahidi kunipa makonde kadhaa yaliyo niingia
vizuri sehemu mbali mbali za mwili wangu
“Eddy nakuomba uwe mpole kumbuka hapa tupo shule”
Madam
Mery alizungumza kwa upole huku nikiondolewa eneo la tukio na waalimu
wapatao wanne na kwajinsi nilivyo na nguvu na iliwalazimu kutumia nguvu
nyingi katika kunizuia kwenda kuendeleza ogomvi na mkuu wa shule
“Wewe
kijana mshenzi sana hujafunzwa huko kwenu hadi unapigana na mume wangu
na nitahakikisha shule huna wewe mpumbavu mkubwa weee”
Mke
wa mkuu wa shule alizungumza maneno yaliyozidi kunipandasha hasira
laiti angejua mumewe kitu alicho toka kukifanya jana usiku wala asinge
zungumza ujinga anao uzungumza
“Sawa waalimu wangu nimewaelewa ngoja mimi niondoke zangu naombeni muniachie”
Nilizungumza kwa upole na kuwafanya waalimu wa kiume walio nishika
kuniachia taratibu na huku wakiniomba niondoke sehemu ya eneo la
shule.Kwa haraka nikamsukuma mwalimu wa mbele yangu akaanguka chini
nikapata nafasi ya kukimbilia eneo alilopo mkuu wa shule na nikamchomoa
katikati ya watu wanao mpa pole na kumpiga kabali moja takatifu
iliyotupeleka hadi chini ardhini na watoto wa mjini wenyewe tunaiita
kabala ya mbao na kuwafanya walinzi na waalimu wa kiume kuanza kuushika
mkono wangu na kuanza kuuvuta kwa nguvu ili kuyanusuru maisha ya mkuu wa
shule.Wakafanikiwa kunichomoa huku mwili wangu ukiwa umejaa jasho jingi
huku misuli ya mwili mzima ikiwa imetuna kiasi kwamba mtu aliyezoea
kuniona kwenye mazingira ya kawaida atabisha kuniona kwenye hali ya
hasira niliyo nayo sasa na atasema sio mimi
Mke
wa mkuu wa shule akaanza kumfuta futa mumewe mchanga kwenye uso wake
kiasi kwamba baadhi ya wanafunzi wakaanza kumcheka kwa jinsi anavyo
tisha sura kwa kuchafuka.
“Oya Eddy tutakuchukulia hatua za kisheria sisi kama shule”
“Tea
na wewe mwalimu wa nidhamu ninakumind kama nini sasa na wewe ingia
kwenye kumi na nane zangu……Wewe unajua huu ugomvi umetokea wapi au
unazungumza zungumza kumpa bichwa huyo choko wenu sifa……”
Nikasimama
kwenye sehemu iliyopo juu na kuwafanya watu wote wanitazame kwa umakini
huku wakinisikiliza akiwemo mkwe wa mkuu wa shule
“Huyo
mzee wenu anahabari za kiseng* sana….Kazi yake ni kuwachukua wanafunzi
wa kike na kwenda nao kwenye mahoteli makubwa na kufanya nao
mapenzi.Ushahidi ninao na kama mwalimu yoyote atake bisha nitautuma
kwenye wizara ya elimu tuone kama hii shule haito fungiwa”
Nilizungumza
na kumuona Salome akijikatiza katikati ya wanafunzi na waalimu na kuja
kupanda sehemu niliyo simama mimi huku akionekana kuwa na asira
kali.Nikamtazama kwa jicho kali kiasi kwamba akatulia na kuzidi
kuwafanya wanafunzi kuzidi kuongezeka wakitokea mabwenini na madarasani
wakitaka kujua ni nini kinacho endelea
“Hapa
nina gazeti linaelezea mambo ya huyo mzee aliyo yafanya jana usiku
isitoshe alitaka kuniua kwa kunipiga na bastola ila kwa bahati mbaya
akampiga mpenzi wangu na sasa hivi ninavyo zungumza amelazwa
hospitalini”
Minong’ono
ya wanafunzi ikaanza kutawala eneo tulilopo na nikaanza kazi ya
kuwanyamazisha wanafunzi wezangu na kumfanya mkuu wa shule kuzidi
kunitumbulia mimacho ya hasira na kila alipotaka kuondoka mke wake akawa
anamzuia asiondoke
“Ngoja
niwasomee habari ya hili gazeti na mukiwa amuamini nitawawekea video au
picha za huyo mzee muone mambo mauvu anayo yafanya…….Kichwa cha habari
cha hili gazeti kanasema HEAD MASTER AUA KISA MAPENZI habari ukurasa wa
pili ianasema hivii….Mkuu wa shule moja jina tunalihifadhi anajiukuta
akiangukia kwenye mikono ya polisi baada ya kumpiga risasi”
Nikapunguza
sauti ya kulisoma gazeti kwani kitu kilicho andikwa kwenye gazeti
kilianza kunichanganya kidogo na nikazidi kukisoma kimya kimya bila mtu
kusikia
“Binti
mmoja na kumuua kabisa.Muobgozaji wa filamu hiyo inayoitwa SCONGA LOVE
imeshirikisha wasanii wengi maarufu kutoka nje na ndani ya mipaka ya
Tanzania.Star wa filamu hiyo ambaye amecheza kama mkuu wa shule
inasemekana ameweza kuziteka hisia za wasanii wezake alio wafanya nao
kazi.Muandishi wetu alikutana na msanii huyo na mahojiano yalikuwa hivi”
Nikanyanyua
macho yangu na kuwatazama wanafunzi na watu wengine wakisubiria
niwasomee kilicho andikwa ndani ya gazeti hilo.Gafla sauti ya Salome
ikaanza kusikika kwa sauti ya juu na kunifanya nimtazame
“Huu
ndi mwisho wa manyanyaso ya wasichana wa kike kwenye hii
shule…..Waalimu wengi hapa shule hututumia sisi kama vituliza nyeg* japo
wana wake zao na wengine magirl friend zao……Mfano mzuri ni mimi.Jana
asubuhi nilimuomba mwalimu wa zamu Pass(Ruhusa) ya kwenda kununua
matumizi yangu binafsi kabla sijatoka getini mkuu wa shule akaomba anipe
lipfti kwenye gari lake hadi mjini.Sikuwa na hiyana zaidi ya kukubali
kutokana tumememzoea kama baba yetu wa kimwili na kiroho”
Salome
alizungumza huku machozi yakimwagika na kunifanya na mimi niungane na
wanafunzi wengine kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu
“Basi
tukiwa ndani ya gari alipandisha vioo vyake vya gari lake na kuanza
kunitongoza huku akidai atanipa kila nitakacho taka ikiwemo kunivujishia
mitihani ya nusu mwaka kwa sisi A LEVEL……….Nilikataa na mwenzangu
akazidi kuliendesha gari lake kwa kasi na sikuweza kushuka kwani hata
mjini kwenyewe alinipitisha na tukafika kwenye moja ya hoteli na
akanitolea bastola na kuniambia endapo nitakataa kushuka ndani ya gari
ataniua.Sikuwa na ujanja zaidi ya kufanya kama alicho
niagiza.Tukapitliza moja kwa moja kwenye chumba na head master
akanilazimisha nifanye naye mapenzi bila kinga…….Na isitoshe
aliniingilia kinyume na maumbile”
Mwili
mzima ukafa ganzi nikabaki niemeduwaa huku wanafunzi wengie wakianza
kutokwa na machozi wakimuonea haruma Salome.Ukelele mkali ukasikika
katikati ya wanafunzi na ni mke wa mkuu wa shule alizidi kupiga makelela
huku akiongea kichaga na kumpiga piga mumewe kwenye kifua
“Baba Evance mtoto wa watu umeshamuua wewe si unajijua kuwa sisi ni waadhirika ni kwanini sasa umefanya hivyo baba Evance”
Salome
baada ya kuyasikia maneno ya mke wa mkuu wa shule akalegea mwili wake
na kabla hajafika chini nikamnyaka na kumlaza taratibu na vilio vya
wanafunzi wa kike vikaanza kutawala huku wengine wakidai wametembea na
mzee huyo bila kinga na nimiongoni mwa wanafunzi walio ambukizwa virusi
vya ukimwi.Waalimu wa kiume wakaanza kumchukua mwalimu mkuu na
kumuingiza ndani ya gari la shule na wakaondoka kwa kasi katika eneo la
shule kwani wanafunzi walianzisha vurugu za kuwarushia mawe
“NANI YUPO PAMOJA NAMI”
Wanafunzi
karibia wote wakanyoosha vidole juu akiwemo rafiki yangu John ambaye
alikuja wakati wa mwisho mwisho wa tukio na ninavyo mjua alikuwa
ametoroka.Wanafuzni wakaanza kurusha mawe kwenye ofisi za waalimu na
kuvunja vioo,nikamnyanyua Salome nikisaidiwa na wezake na tukamuingiza
ndani ya gari langu huku John akiingia kwenye siti ya upande wangu huku
akijichekesha chekesha.Nikawasha gari na kwa kasi ya hali ya juu
nikanza kufwata njia ilipo elekea gari la shule kutokana katika eneo
hiko kuna njia moja tu ya kutokea.Kwa mwendo kasi wa gari langu nikaanza
kuliona gari alilopanda mkuu wa shule kwa mbali likikata kona kusoto
kushika njia ya kuelekea porini kwenye migomba mingi
“Eddy na huyo Salome tunakwenda naye wapi?”
“Huko huko”
“Huko huko wapi akitufia mtoto wa watu itakuwaje?”
“Potelea pote ila cha msingi nilazima mkuu wa shule alipe kwa hili”
“Eddy mtu mwenyewe mbona kama haemi”
“John hembu niachie kelele”
Johnalizungumza
kimasihara kiasi kwamba ninaona anazidi kunichanganya,Simu yangu
mfukoni ikaanza kuita na ninamba ngeni ndio inayo ingia ikanilazimu
kuipokea na kuweka loudspeaker
“Eddy mume wangu uko wapi?”
Ilikuwa ni sauti ya Sheila ikizungumza kwa upole
“Baby usijali ninakuja…hii namba ni ya nani?”
“Ni namba ya nesi nimemuomba”
“Umeshakula baby?”
“Ndio mume wangu……nakuomba ndani ya dakika kumi uwe umefika hapa la sivyo nitameza vidonge nijiue kabisa”
“Mke wangu usiseme hibyo”
“Nasema hivyo kutokana nina hamu na wewe na ninahisi upo na mwanamke mwengine”
“No baby naomba usinifikirie vibaaya”
“Sawa ila fanya hivyo nakuesabia dakika mume wangu”
“Sawa”
Nikakata
simu na kuzidi kuongeza kasi ya gari langu hadi nikafanikiwa kulipita
gari alilopo mwalimu mkuu kisha nikalisimamisha gari langu gafla kitendo
kilichomfanya dereva wa gari alilopanda mwalim mkuu kunikwepa na
kugonga mti mkubwa uliopo pembeni ya barabara nagari lao likasimama
kiasi kwamba ndani ya dakika mbili hapakuwa na mtu yoyote aliye shuka
kutoka ndani ya gari lao.Nikashuka na kuitoa simu yangu na kuanza
kurekodi tukio moja baada ya jengine hadi ninafika kwenye gari la shule
nikamkuta dereva wa gari hilo akiomba msaada wa kutolewa ndani ya gari
hilo hii nibaada ya kubanwa na mskani wa gari kwenye kifua.Kitu kilicho
nishagaza sikuweza kumuona mwalimu mkuu wala waalimu wengine wa kiume
walio toroka eneo la shule
“Mkuu wa shule yupo wapi?”
“Ni…liwas…shusha…..njiani”
“Wapi?”
“Kul…e kwenye shamb…..a la migomba”
“Fuc*”
Nikamuacha
derava akiendelea kubanwa na mskani wake na nikaingia ndani ya gari
huku John akifwatia kwa nyuma na kuingia ndani ya gari na kufunga mkanda
“Eddy si tungemsaidia jamaa wa watu”
“Siwezi kusaidia mijitu mipumbavu kama yeye”
“Kwa nini?”
“Hii vita yeye haimuhusu kilicho mfanya aingilie ni nini?”
“Eddy kuwa na roho ya kibinadamu yule jamaa yupo powa sana huwa……”
“JOHN KAMA UNATAKA KUMSAIDIA SHUKA NDANI YA GARI LANGU NA UENDE UKAMSAIDIE”
Nilizungumza
kwa sauti kali iliyo jaa hasira kiasi kwamba John akastuka na kukaa
kimya,Nikageuza gari na kabla sijafika umbali kutoka lilipo gari la
shule lilipo pata ajali nikasimamisha gari
“Eddy nishushe nikamsaidie jamaa wa watu”
“Powa shuka”
John
akashuka ndani ya gari na mimi nikaendelea na safari ya kurudi mjini
huku gari nikiliendesha kwa mwendao wa kasi ili nimuwahi Sheila aliye
nipa dakika la sivyo anaweza kufanya kitu kibaya cha kujiua.Kitendo cha
kufika hospitli nayo simu yangu ikaita kwa namba ile aliyo nipigia
Sheila kwa mara ya kwanza nikaipokea
“Eddy mume wangu hutaki kuja eheee?”
“Nipo hapa nje”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
“Sawa”
Nikamuita
nesi mmoja na kumuonyesha Salome tuliye mlaza siti ya nyuma na kumuomba
amtoe na kumfanyia huduma ya kwanza.Nikapitiliza moja kwa moja hadi
chumba alicholazwa Sheila na kumkuta akiwa ana wasi wasi
“Baby mbona umechelewa”
Nikaanza
kumuadisia Sheila kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho wa tukio lilivyo
tokea ila nilimficha juu ya uwepo wa Salome kwenye hospitali hiyo
“Sasa huyo mkuu wa shule yeye yupo wapi?”
“Sijui yupo wapi na mbaya zaidi jana alipo toka kufanya tulio la kukupiga risasi polisi wakamuachia huru”
“Mmmm mume wangu ninakuomba umpotezee”
“Siwezi kufanya hivyo yule mzee anatabia chafu na isitoshe anawaambukiza wanafunzi wa kike HIV kimakusudi”
“Weeee”
“Ndio hapa shule wanafunzi wengi wa kike nimewaacha wakili na nahisi ametembea na wengi sana”
“Mmmm kweli huyoo si mtu wa kuacha uraiani.Sasa wewe kama wewe umeamuaje?”
“Hi video nitaituma kwa mama kisha atajua nini cha kufanya”
“Ngoja kwanza ukimtumia mama yeye akikuuliza ulifwata nini hotelini utamjibuje?”
“Nitajua cha kumuambia mimi mama yangu hana neono”
“Mmm mimi ninakushauri usimtumie ni bora ukaituma kwa huyo waziri wa elimu”
“Umesha kula?”
“Ndio na wamenichoma sindano ya kukausha kidonda”
“Wamekuchomea wapi hiyo sindano”
“Kwenye makalio”
“Kwahiyo wamekushika mpododo?”
“Bwana Eddy hembu acha utani wako”
“Ngoja nikachukue msosi tangu jana tulipo kule njiani hadi sasa hivi sijaweka kitu mdomoni”
“Sawa mume waangu ila usichelewe kurudi”
Nikamnyonya lipsi Sheila na kutoka nje chumba na kwenda alipo lazwa SALOME na kukuta madaktari wakimshughulikia
“Dokta amepata tazizo gani?”
“Amepata mstuko wa moyo”
“Mmmm kwahiyo itakuwaje?”
“Ndio tunamshuhulikia kuurudisha moyo wake kwenye hali yake ya kawaida”
“Sawa dokta kila kitakocho endelea unijulishe kwenye hii namba”
“Sawa”
Nikamuachia
daktari namba yangu ya simu kisha nikatoka na kwenda kwenye mgahawa wa
karibu na hospitali na nikaagiza chakula na kuanza kula taratibu huku
nikitafakari ni nini nifanye juu ya ushaidi wa kumkamata mkuu wa
shule.Tv(Luninga) iliyopo kwenye mgahawa Chaneli Ten ikaonyesha habari
iliyo wafikia kwa wakati huo(BREAKING NEWS) na kunifanya niache kula na
kuitazama kwa umakini.Nikashuhudia jinsi askari wakijitahidi kutuliza
fujo zinazo endelea shuleni kwetu huku ofisi za waalimu zikiwa
zinateketea kwa motoTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
