Max amejitokeza kusema hayo baada ya Ruby kutangaza kujitoa kwenda kutumbuiza kwenye Fiesta Mwanza licha ya kusaini mkataba wiki chache zilizopita. Ruby ameitupia lawama Clouds na management ya THT kuwa hawathamini wasanii.
Lakini Max anadai kuwa kwa wasiomjua Ruby wanaweza kuhisi anaonewa lakini wanaomjua wanafahamu alivyo na matatizo.
“Ruby ni msichana ambaye hawezi kuishi na watu wote vizuri kutokana na the way anavyojiweka yaani mtu fulani hivi wa ususa susa na kukera kera, vitu ambavyo watu wengi hawapendi kufanyiwa kibinadamu japo ana uwezo mkubwa wa kuimba,” Max ameiambia Bongo5.
“Na kwa upande mwingne tunasema bado hajakuwa kiujumla,” anasema Max.
“Kwa sababu inasikitisha sana ..mama yako alokulea ukaanza kumtukana, si utapata laana? Hata kama kakukosea waswahili wanasema mama ni mama tu hata awe chizi atabakia kuwa mama. Uamuzi aliochukua anaweza akaona amefanya kitu poa lakini nina uhakika amefanya kitu ambacho atakuja kujuta maisha yake yote,” amesisitiza.
“No way out…jiulize wasanii wangapi wapo Clouds wasanii wangapi wapo THT na ushawahi kusikia wanalamika eti pesa ndogo wanayolipwa kwenye show au kaz yoyote! Mimi nIpo pale THT inaenda 1 year and a half sasa, sijaona mtu akidhulumiwa,sana labda utachelewa kulipwa tu.”
“Tukienda mbali Ruby amekuwa akitukosea hadi sisi wasanii wenzie, imagine tuko wote kituo kimoja halafu hatuongeleshani, huongei na wenzio, bingwa wa kushushua wasanii wenzio kutukana yaan she is out of discipline na kibaya zaidi anasahau kuwa mabosi walikuwa wakimfichia machafu yake anayoyafanya ilimradi tu brand yake iendelee kukua. Anatukosea wala haadhibiwi, nafikiri ndio amejisahau na kujiona kuwa hakuna kama yeye sababu anajua kuimba na vile show zote alikuwa hakosi basi ndio akajihakikishia hivyo na kujikuta na yeye commando. Huwezi kujicompare na commando [Lady Jaydee] she is a legend, hayo ni mambo ya wakubwa yaan Ruby ni worst,” amesisitiza Max.
“Niulize kitu, unaweza ukasaini mkataba kabisa wa show halafu imebakia masaa show ifanyike ndio unasema eti huwez kufanya show maslahi maduchu? Sasa ulisaini ili iweje? Hukusoma pale pale mkataba ulipopewa? Mazoezi yote kafanya ya show na kwenye social anaandika kabisa kwamba yuko excited na kuchukuliwa Fiesta na kusaini, few hours before unazngua! Mimi nafikiri cha kumshauri Ruby kwa sasa angerudi tu kanisani aendelee na nyimbo za dini, atapata vihela huko maana na kanisani kwenyewe nako pia alichafua akapewa laana ya kanisani.”
Bongo5
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )