Naibu Balozi wa China nchini
Bw.Gou Haodong akizungumza jambo na wanafunzi wa kitanzania waliopata
ufadhili wa kwenda China kusoma masuala ya mafuta na Gesi leo jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof.
Sospeter Muhongo akizungumza na watanzania(hawapo pichani) waliopata
ufadhili wa kwenda China kusoma masuala ya mafuta na Gesi.
Waziri wa Nishati na Madini Prof.
Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waliopata
ufadhili wa kwenda china kusoma masuala ya Mafuta na Gesi leo jijini Dar
es Salaam.Pichani watanzania hao wakionyesha nyaraka za udhamini huo.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
…………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi
MAELEZO.
Dar es Salaam
26.8.2016
WAZIRI wa Nishati na Madini Prof.
Sospeter Muhongo amekabidhi nyaraka za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi
20 wa kitanzania wanaokwenda kusoma fani za mafuta na gesi katika ngazi
za uzamili na uzamivu nchini China.
Watanzania hao 20 wamepatikana
kutokana na mchujo na Wizara hiyo ukihusisha watanzania 89 kwenye ngazi
mbalimbali za elimu nchini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
nyaraka hizo leo Jijini Dar es Salaam, Prof. Muhongo alisema kuwa wizara
ya Nishati na Madini imekuwa ikisomesha vijana wa kitanzania nje ya
nchi kwa ajili ya kusomea masuala ya mafuta na gesi.
“Serikali ya China imetoa nafasi
kwa vijana wa kitanzania kusoma nchini mwao na kwa jinsi ilivyo tukaona
ni vyema tuzitangaze nafasi hizi kwa Watanzania wote kupitia wizara yetu
ili waweze kuisaidia nchi yao na baada ya mchujo leo hii tunawakabidhi
nyaraka zao za masomo” alisema Profesa Muhongo.
Aidha Profesa Muhongo aliwataka
vijana hao kuitumia vyema nafasi waliyoipata na kuhakikisha wanasoma kwa
bidii kwani nchi inahitaji wataalamu wa kutosha katika sekta ya mafuta
na gesi ambayo inakua kwa kasi ya haraka nchini.
Kwa upande wake Naibu Balozi wa
China Nchini Bw.Gou Haodong amewaasa watanzania hao kusoma kwa bidii
wakiwa nchini china na kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kitaaluma.
Pia amewaasa kuhakikisha wanawafundisha watu wa china utamaduni wa mtanzania na wawe mabalozi wazuri wa nchi yao.
Serikali ya China inatoa ufadhili
wa nafasi 20 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano kwa watanzania ili
kujifunza masuala ya Gesi na Mafuta nchini mwao kupitia Wizara ya
nishati na madiniTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )