Featured
Loading...

BREAKING NEWSS::UFISADI UVCCM ,HIVI NDIVYO M/KITI WA UVCCM ALIVYOKUWA AKIJIPATIA FEDHA KWA NYARAKA ZA KUGHUSHI ZA USALAMA WA TAIFA


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya anatuhumiwa kughushi nyaraka za Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na kuzitumia kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara mkoani Arusha.
Aidha, taarifa hizo ambazo hazijathibishwa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi wa CCM na serikali mkoani Arusha walikuwa wakifahamu kitendo hicho lakini wakakifumbia macho.
Huu hapa chini ni ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukielezea jinsi mwenyekiti huyo alivyokuwa akifanya mambo yake.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Arusha anadaiwa kufanya utapeli na kujipatia mamilioni ya shilingi kwa kugushi nyaraka za usalama wa taifa na kujitambulisha kuwa ni afisa wa idara hiyo nyeti.
Taarifa kutoka vyazo vya kuaminika, inaeleza kuwa Sabaya amekuwa akijitambulisha kuwa ni afisa wa usalama wa taifa na kutumia nafasi hiyo kutapeli wafanyabiashara mbalimbali hasa wamiliki wa hotelini na wengine akiwahaidi kuwatafutia kazi katika ofisi nyeti za umma.
Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni diwani wa kata ya Samabashi wilaya ya Arumeru, kupitia chama cha mapindizi (CCM), anadaiwa kutumia nafasi ya kughushi ya usalama wa taifa kufanya utapeli, kwa kulindwa na baadhi ya vigogo wa CCM mkoani humo.
Baadhi ya vigogo wanaodaiwa kufahamu utapeli wa Sabaya na kuufumbia macho ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Arusha, Catherine Magige, na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia chama cha mapinduzi jimbo la Arusha mjini Philemon Mollel. Wapo pia viongozi wakuu wa serikali na baadhi ya watumishi wa umma wanaodaiwa kumficha Sabaya. Inadaiwa pia kuwa sababu ya kugoma kuondoka ofisini kwa aliyekua Katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel ilikua ni kumlinda Sabaya.
Mmoja wa viongozi wa UVCCM wilaya ya Arusha mjini asiyekubaliana na utapeli wa Sabaya amesema “huyu ndugu anatumia nafasi yake vibaya lakini analindwa na wakubwa. Ameghushi kitambulisho cha usalama wa taifa wakati yeye si mtumishi wa idara hiyo, na anatumia kitambulisho hicho kufanya utapeli lakini hakamatwi na viongozi wanajua.
Katika tukio moja Sabaya anadaiwa kutumia kitambulisho cha idara ya usalama wa taifa kumtapeli binti mmoja mjini Arusha kiasi cha shilingi milioni 7 kwa ahadi ya kumpatia kazi katika migodi ya Tanzanite iliyopo Mererani Arusha. Licha ya kutapeliwa kiasi hicho cha fedha binti huyo pia aliombwa rushwa ya ngono japo alikataa.
Katika kisa kingine ndugu Sabaya anadaiwa kulala hoteli moja jijini Arusha ijulikanayo kama “Sky Way Hotel” kwa muda wa siku 6 lakini akakataa kulipa. Alipoulizwa alidai yeye ni afisa wa idara ya usalama wa taifa hivyo hawezi kulipa.
 
Uongozi wa hoteli hiyo ulimzuia kutoka hadi akamilishe kulipa deni hilo lakini Sabaya aliendelea kusisitiza kuwa yeye ni Afisa usalama wa taifa hivyo hatakiwi kulipa. Pia aliutishia kwamba wakiendelea kumsumbua ataifunga au kuwanyang’anya leseni ya kuendesha hoteli hiyo.
Hata hivyo uongozi wa hoteli hiyo haukutishwa na kuamua kumsachi ambapo walikuta hana fedha taslimu lakini walifanikiwa kumnyang’anya vitambulisho vyote na kadi za benki. Kisha wakamfungulia kesi katika kituo cha polisi kati yenye jalada AR\RB5044\2016 ambapo pia waliwasilisha vitambulisho vyake walivyomnyang’anya.
Baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Mwenyekiti huyo alienda kujisalimisha polisi na kulipa deni alilokua anadaiwa na hoteli hiyo kiasi cha shilingi 309,400 na polisi wakamkabidhi vitambulisho vyake. Jambo la ajabu ni kwamba polisi walimrudishia hadi kitambulisho cha kughushi cha usalama wa taifa anachokitumia kutapeli.
Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mtui alisema Mwenyekiti huyo hana makazi rasmi na amekua mtu wa kulala nyumba za wageni, na kufanya starehe kwa pesa anazopewa na vigogo wa CCM na serikali ambao wamekua wakimtumia kuchafua baadhi ya viongozi wa serikali na makada wengine ndani ya CCM”
  Uchunguzi uliofanywa imebaini kuwa katika kituo cha polisi kati, Sabaya amewahi kufunguliwa kesi 4 na watu tofauti kwa madai ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lakini hakuna hata kesi moja aliyopelekwa mahakamani.
Baadhi ya viongozi ndani ya CCM mkoa wa Arusha wanajitahidi kuzima habari kuhusiana na utapeli wa Sabaya kwa lengo la kumtumia kujinufaisha kisiasa. Viongozi hao wamesikika mara kadhaa wakipendekeza Sabaya kugombea uenyekiti wa UVCCM taifa licha ya tuhuma lukuki zinazomkabili.
 

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top