Mamba alitolea mfano wasanii wanazungushwa mikoani kwenye tamasha la fiesta na kuambulia ujira mdogo, huku akisema pesa wanayopata kwenye hilo tamasha huishia hukohuko mikoani na hurudi dar wakiwa wamepayuka hawana kitu mfukoni
Dudu alisema hayo akipokuwa kwenye kipindi cha usiku cha FRIDAY NIGHT LIVE... FNL kinachorushwa na EATV
Alienda mbali zaidi kwa kumpongeza msanii mwenye kipaji anayekuja juu ruby kwa kusema ametoka kwenye minyororo ya wafu FM akawasihi na wasanii wengine wamuige ruby kwani ameonesha mfano
Akionekana mwenye afya km alivyokuwa zamani, amesema wafu fm hawajapiga nyimbo zangu kwa miaka sita sasa lakini sijatetereka naendelea na maisha yangu kama kawaida
Wakati akiendelea kuwatolea uvivu clouds fm mtangazaji wa kipindi hicho sam misago alitumia mbinu ya ziada kumtoa kwenye kile akichokuwa nacho moyoni
Hata hivyo alipongeza redio ambazo zipo chini ya IPP km East africa radio, radio one, capital fm na kusema hajawahi kuombwa pesa na mtangazaji au dj yeyote wa kituo hicho ili wimbo wake uchezwe hewan
Amevitaka vituo vingine kuiga vyombo vya ipp media
Kwa maneno ya dudu baya ni dhahiri wasanii wengi ni watumwa wa baadhi ya media house
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )