Serikali imepeleka wataalamu wa Jiolojia katika eneo lililokumbwa na
tetemeko Bukoba ili wakafanye utafiti wa kina kuhusu tetemeko hilo.
Kwa kuwa kitovu cha tetemeko hilo kiko chini sana ya ardhi (Km 10) na
kwa kutafasiri umbile la mawimbi ya tetemeko hilo yaliyonakiliwa na
vituo vya kupimia matetemeko ya ardhi inaonekana kuwa tetemeko hilo
limetokana na misuguano ya mapange makubwa ya ardhi iliyopasuliwa na
mipasuko ya ardhi mithili ya mipasuko kwenye bonde la ufa. Kwa kuwa eneo
lililokumbwa na tetemeko la ardhi liko karibu na mkondo wa magharibi wa
bonde la ufa la Afrika Mashariki inakisiwa kuwa mtetemo huu
umesababishwa na kuteleza na kusiguana ka mapande ya miamba juu ya
mipasuko ya ardhi ya bonde hilo la ufa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )