Featured
Loading...

List ya miji 10 ya gharama zaidi kuishi barani Afrika

 
Gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku katika miji mbalimbali duniani, shirika la Mencer limeziorodhesha gharama za bidhaa na huduma 200, pamoja na malazi, huduma za chakula, starehe, usafiri wa umma na huduma za kijamii na kupata orodha ya miji inayoongoza kwa gharama zaidi za kujiendesha kimaisha.
Hii ni list ya miji kumi iliyotajwa kuongoza kuwa ghali zaidi kuishi barani Afrika.
10-ABUJA
Mji mkuu wa Nigeria  na wenye mpangilio mzuri pamoja na  wakazi zaidi ya 979,876 na ulianza kujengwa kwenye miaka ya 80, ukiongelea Abuja Rais wa kwanza wa Afrika Kusini alishawahi kujisemea …”kwanini tuende ulaya wakati tunayo ulaya hapahapa” akimaanisha maisha ya Abuja hayatofautiani na nch za ulaya kutokana na gharama kubwa za maisha.
9- Conakry ni mji wa kibiashara na mkubwa zaidi nchini Guinea  unatajwa kuwa kati ya miji ya gharama zaidi kuishi katika bara la Afrika, kwa bahati mbaya licha ya mji huu kuwa mji wa gharama bado miundombinu yake sio mizuri katika baadhi ya maeneo.
Conakry
8-Bamako ni mji mkuu wa Mali na moja kati ya miji ya gharama Afrika makampuni mengi ya kigeni na mashirika ya misaada yameweka makazi yao katika mji huo. Watu hawa huhitaji kuishi kama nchi za ulaya hii imeongeza gharama za kimaisha mjini humo.bamako-city-skyline
7- Brazaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na matajiri ama watu wenye pesa ndio wenye uwezo wa kukabiliana na gharama za  maisha kutokana na bei za matumizi kuwa juu kulinganisha na miji mingine ya Afrika.
brazzaville-city
6- Lagos ni mji mkubwa wa kibiashara nchini Nigeria na matajiri wengi wanaishi katika visiwa vya jiji hilo,  foleni za magari ni kitu cha kawaida katika mji huu wa gharama barani Afrika.
Lagos-Nigeria
Lagos-Nigeria
5- Kinshasa, mji huu una zaidi ya watu millioni 4 ikiwa ni mji mkubwa wa kibiashara nchini Congo sifa zake ni pamoja na usalama wa uhakika kwa wageni.
Kinshasa- Congo
Kinshasa- Congo
4- LIBREVILLE ni mji mkuu wa Gabon unaotajwa kuwa na wakazi zaidi ya laki tano,  Gabon ni moja kati ya nchi zenye utajiri wa maliasili pia inapokea misaada mingi kutoka kwenye nchi zilizoendelea. Mji huu unasifika kwa kuwa na kumbi za starehe (klabu) za gharama kubwa.
libreville-skyline
Libreville-Gabon
3- VICTORIA ni mji mkuu wa Shelisheli umetajwa kuwa kati ya miji ya gharama kubwa kuishi Afrika , alishawahi kufika Prince William wa Uingereza na mke wake wakati wa  Honeymoon na iliripotiwa kwamba kwa usiku mmoja walilipia chumba kwa dola 5,000 jinsi gani ambavyo hotels na nyumba za ufukwe huo ni ghali.
Victoria-Shelisheli
Victoria-Shelisheli
2- N’Djamena ni mji mkuu wa Chad, ingawa umetajwa kuwa mji wa pili ambao ni ghali zaidi kuishi barani Afrika, hauna miundombinu ya kutosha, hakuna reli wala bandari katika mji huu.
N'Djamena
N’Djamena
1- LUANDA, mji mkuu wa Angola na pia mji ghali zaidi kuishi kuliko yote barani Afrika na pia upo katika list ya miji ghali zaidi kuishi duniani mji huu kupanga nyumba kwa euro 10,000 mpaka euro 30,000 ni kitu cha kawaida kwenye mji huu.
Luanda
Luanda

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top