Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Na
jinsi ninavyo ogelea kwenda mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi
kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni
papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye
kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta
nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo
Endelea...
....Gafla
nikasikia milio mingi ya risasi iliyoanza kunichanganya hata mfumo wa
kuogelea ukabadilika nikatamani maji ya bahari yabadilike na kuwa
mchanga ili miguu yangu ipate uwezo wa kukimbia ila hikuwa hivyo zaidi
ya milio kuzidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kwakiweza sikujua hata
ni wapi inapo tokea,maji yakabadilika na kuanza kuwa na rangi nyekundu
nikageuka nyuma na kukutana na boti iliyo wabeba watu wapatao wanne
wenye bunduki na pembeni nikamuona papa aliyekuwa akinifwata akielea
elea juu ya maji akiwa amekufa.
Jamaa
wenye boti yao wakaisogeza hadi pembeni na kunitazama kwa muda kisha
wakanipa mkono na kunivuta kwa nguvu huku buinti mdogo akuwa
mgongoni,wakanipa kitaulo cha kujifunga na kunza kumfwata mama ambaye
tayari alisha fika mbali kutoka sehemu ambayo nilikuwepo mimi.Jamaa
mmoja alizungumza na simu na sikuielewa luga yake kutokana anazungumza
kikabila kisha akakata simu.Wakaisogeza boti yao hadi alipo mama na
wakamvutia ndani ya maji.Nikawaona jamaa wakinong’onezana na kisha
wakagongeana mikono ikatubidi mimi na mama tutazamane.
“asanteni ka masaada wenu”
Mama alizungumza huku akiwatazama usoni
“musijali kwa hilo”
Jamaa wakaonekana kutawaliwa na furaha ambayo hadi wakati huu sikujua ni ya nini
“mbona munafurahi?”
“tunafurahi kwa maana tumesha kuwa ni matajiri”
“matajiri wa nini?”
“kuna
tangazo lilikuwa linatolewa kwa mtu atakaye fanikisha kukupata wewe
atapewa dola milioni mbili za kimarekani na baba yako na sasa ni mwezi
wa tatu ndio sisi tumekupata”
Nikatabasamu ila ikawa ni tofauti kwa mama ambaye nahisi kuwa anajua ni mume wake mzee godwin
“eddy waambie wanipige risasi ili nife sipi tayari kurudi tena mikononi mwa baba yako”
“mama sio baba wa tanzania?”
“unataka kusema wewe baba yako yupi huyo mwenye roho ya kibinadamu atakaye toa pesa yake ili amzawadie mtu?”
“mama
sio baba unaye mjua wewe…tambua kuwa ukweli wote ninauju na
ninamshukuru mungu kuwa nimempata baba yangu ambaye yeye ndio damu yeke
japo amepitia yaliyo mengi ila ninamshukuru mungu yupo hai”
Mama
akabaki kimya huku macho yake yakiwa chini akimtazama mtoto tuliye
mlaza chini,tukaona boti nyingine kubwa ikija na kusimama karibu na
sehemu ilipo boti hii ndogo,wakatuwekea kingazi na tukaanza kupanda na
kuingia kwenye boti kubwa iliyo kuja na jamaa watatu wakingia na
kumuacha mwezao mmoja kwenye boti ndogo.Ndani ya boti wakatupa makoti
makubwa kwa ajili ya kuzui baridi kali iliyo kuwa ikitukung’uta.
Wakampa
msichana mdogo huduma ya kwanza na sisi wakatupatia vyakula na chai ya
moto kutoa njaaa tumboni.Mimi wakanihudumia kwenye sehemu niliyo
jeruhiwa na jiwe kisha wakanipa suruali mpaya,nikavua kitaulo nilicho
pewa na kuivaa suruali hii.Boti ikazidi kusonga mbele huku moyoni mwangu
nikijawa na amani tele ya kuweza kumpata mama yangu na kilicho salia ni
kuwaunganisha baba mzazi na mama.
“samahani kaka nyinyi ni kina nani?”
“sisi
ni wavuvi wa samaki wakubwa sasa yule papa tuliye muua tulikuwa
tunamkimbiza alitusumbua sana na pale tumemuacha yule mwezetu akilinda
sisi tutamrudia kumchukua na boti nyingine”
“sawa”
Tukafika
ufukweni na jamaa wakatupeleka kwenye moja ya hotel isiyo mbali sana na
bahari na kutuchukulia chumba,wakamchukua daktari maalumu na kuja
kutuhudumia.Tukakaa hotelini kwa wiki moja tukijitahidi kuirudisha miili
yetu katika afya zake za kawaida kwani kwa muonekano tulio nao ninaweza
kujifananisha na misukule.Mudu wa wiki moja kukatika afya yangu
ikarejea kama awali japo sio sana ila kidogo niliweza kusimama mbele ya
mtu au watu na kujiona ni mtu.
Gharama
zote zikalipwa na mama kutokana na kuwa na akaunti yake ya siri iliyopo
huku afrika kusini na kwakipindi chote hatukuwasiliana na mtu yoyote
zaidi ya jamaa walio tuokoa ambao nao mama aliwakanya wasizungumze
ummbea wa aina yoyote kwa mtu yoyote ili waweze kupata donge lao nono
wanalo lisubiria kwa hamu kubwa kutoka kwa baba yangu mzazi
Msichana
mdogo alilazwa kwenye moja ya hospitali na madaktari wanaendelea na
juhudi za kuweza kumtibu kama ataweza kuzungumza tena ili awe miongoni
mwa mashaidi wa kumuhukumu baba mzee godwin katika kesi ya kuwatumikisha
watu kikatili na kuwakatili katika kuzungumza nao.
“mama unampango gani na baba?”
”nitahakikisha ninamfunga hadi magereza yanabomoka”
“sawa mama je baba yangu mzazi naye una mpango gani naye?”
“mmmm sijui hata ni wapi nitaanzia kwa maana kwa niliyo mfanyia baba yako kidogo yananipa hata ugumu wa kusema ninaanzi wapi”
“ninafurahi kusikia hivyo mama ila kwa hilo ninaomba uniachie mimi kwa maana baba ananipenda sana”
“ila eddy roho yangu imejawa na dukuduku kubwa ambalo sielewi siku ninamkamata godwin nitamfanya kitu gani?”
“hilo
mama wala lisikutie mawazo sana cha msingi ni kuweza kumuomba msamaha
baba yangu ili kama ni maisha yaweze kuendelea kwa amani”
“sawa mwanangu nitafanya hivyo”
“je umewasiliana na serikali ya tanzania?”
“mmmm siwezi kufanya hivyo kwanza kutokana huwezi jua baba yako ana mtandao mkubwa kiasi gani ila nitarudi kimya kimya”
“hapo umesema ila yule daktari wako ni mnoko sana na kama unaweza awe miongoni mwa watu wa kushuhulikiwa”
“kwa nini?”
“ana
vitu vingi sana ambavyo wewe ukimuambia humuambia baba,kwa mfano swala
la kuwa mimi sio mwanaye wewe siku ulipokuwa unamwambia pale sebleni
kama sisi.Yeye kaenda kuyang’aza kwa lile jijambazi ndio maana likatumia
uwezo wake wa kijeshi kufanya mambo ya ajabu kama haya”
“kumbee
hapa ndio ninaanza kupata picha kwa maana siku ambayo waliniteka
hospitali baba yako akawa analalamika kuwa nimemdhalilisha na lazima na
mimi anidhalilishe”
“ndio hivyo mama je ile siku walikupeleka wapi?”
“walinipeleka sehemu moja hivi wala sikujua ni wapi ila nikaja kukutana na binti mmoja aliniambia anaitwa nani vileee…..”
“nani…..?”
“jina
lake limenitoka mara moja alisema na yeye anatokea tanzania na
anakufahamua sana wewe na mumeshirikiana sana kwenye mambo mengi”
“sheila”
“eheee
huyo huyo….Yule binti alinisaidia sana kipindi nipo matesoni kweni baba
yako alinipeleka kwenye jijumba chakavu msituni huko wakanifungia…cha
kushukuru mungu yule binti alikuwa akiniletea chakula kila siku usiku
kwani wao walikuwa wakinipa vyakula vibaya?”
“kina nani?”
“si hilo jibaba lako na watu wake”
“ahaaa ila sio baba yangu”
“basi siku kama mbili zilipita sikumuona sheila sasa sikujua ni wapi walimpeleka binti wa watu sijui walimuua au”
“hawakumuua….Nilikutana naye hapa kipindi cha katikati akiwa amelishwa makaa ya mawe hawezi kuzungumza”
“weeee ndio maana baba yako akaamua kunipeleka kwenye lile jipango na kuniambia kuwa nitalisha keki za moto”
“ndio”
“basi
nakumbuka kipindi ninaingizwa mule sikubahatika kulishwa hayo makaa na
walinipiga na kuninyanyasa sana hadi ikafikia kipindi wakanitenga na
wezanu na kunifungia kwenye kile kijichumba”
“unajua siku ya mwisho unapigwa mimi ndio niliye kusadia kuuziba mwili wako ili nipigwe mimi badala yako”
Mama
akabaki akiwa mdomo wazi na taratibu chozi likamtoka na akanivuta na
kunikumbatia kwa uchungu na machozi yakaendelea kumtoka hadi
akalowanisha bega langu alilo pitishia bega
Niambembeleza
mama hadi akanyamaza na akaniaga na kuingia chumbani kwake kulala na
mimi nikabaki nikitazama tv na nikapitiwa na usingizi kwenye sofa nililo
kaa.Asubuhi kama ilivyo kawaida daktari maalumu anayetuhudumia akaja
kututembelea na kutupa maelezo ya nini tuweze kufanya ili afya zetu
ziweze kuhimarika.Nikwasiliana na jamaa walio tuokoa kili waje
kutuchukua na watupeleke nyumbani kwa baba.
Baada
ya nusu saa jamaa wakawa wamefika na sisi tukawa tayari kwa safri,njia
nzima ndani ya gari mama akawa amenishika mkono huku akiwa na futaha
sana.Tukafika kwenye jumba la baba na nikamuona mama akitazama tazama
kila sehemu
“mama mbona unashangaa?”
“hili jumba lote ni la kwake?”
“ndio”
“amejitahidiTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
