Featured
Loading...

Staa wa Genk katajwa katika list ya kikosi bora cha wiki Europa, Man United hakuna


Usiku wa Septemba 15 2016 michuano ya Europa League ilichezwa barani Ulaya, klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza dhidi ya Rapid Wien ya Austria na kufungwa goli 3-2, magoli mawili ya Genk yalifungwa na Leon Bailey.
Baada ya mchezo huo kumalizika Septemba 16 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kupitia account yao rasmi ya twitter walitoa majina ya wachezaji 11 wanaounda timu bora ya wiki na kwa KRC Genk ametajwa mjamaica Leon Bailey, Bailey anaingia katika kikosi hicho kati ya zaidi ya wachezaji 528 waliocheza mechi za Europa jana.
Kwa upande wa kikosi bora cha UEFA Champions League wametajwa nyota kadhaa wakiwemo wa FC Barcelona lakini kwa upande wa Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid hawakufanikiwa kutoa hata mchezaji mmoja katika kikosi hicho.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top