Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu
wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua
kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha
kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la
Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika
katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"
Mnataarifiwa
kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata
maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye
nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.
Yeyote
aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa
taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.
Aidha,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa
uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari
na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite
kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya
mawasiliano hapo juu.
Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Septemba, 2016
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )