MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA...
Samson alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akimtumbulia mimacho Rahab
“Unaniuliza wewe kama nani?”
“Sio ninakuuliza kama nani, ila nataka kujua unataoka wapi kumbuka kwamba hapa upo kwangu?”
“Hupaswi kujua, mwehu nini wewe?”
Samson akanyanyuka kwa hasira na kumzaba Rahab kibao cha shavuni kilicho myumbisha hadi kikamuangusha chini
ENDELEA...
Rahab
akasimama kwa hasira, akarusha ngumi ambayo Samson aliidaka kwa mkono
wake mmoja na kuachia kibaoa kingine kizoto kilicho myumbisha Rahaba na
kumuangusha chini.
“Sikiliza wewe mwanamke, hata siku mmoja huto weza kunipiga sawa”
Samson
alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Rahab anaye jifikiria
kunyanyuka kutoka katika sehemu aliyo angukia.Rahba akarusha teke
akikusudia kuipiga miguu ya Samson, ila Samsona akaruka juu na kutua
chini, akamnyanyua Rahab kwa mkono mmoja na kumvuta karibu yake
“Nitakuumiza”
Rahab
akajaribu kumpiga Samson igoti cha tumbo ila Samson akawahi kurudi
nyuma, huku akimsukumiza nyuma Rahab.Rahab kwa hasira akarusha teke,
akiwa hewani Samson akamuwahi kwa kupiga tele la mbavu lililo sababisha
Rahab kuangukia kitandani huku akihema
“Usijaribu tena siku nyingine”
Samson
alizungumza huku akimtazama Rahab anaye ugulia maumivu ya mbavu
zake.Rahab akamtazama Samson kwa jicho kali lililo jaa maswali na
mashaka mengi juu ya Samson kwani kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia
sivyo jinsi Samson alivyo
“Wewe ni nani?” Rahab aliuliza
“Mimi ni Samson, au unahisi mimi ni nani?”
“Ninamaanisha unafanya kazi gani?”
“Haaaa mimi si fundi baiskeli”
Samson akafungua boksi lake la kuhifadhia nguo zake, akatoa bastola mbili na kumkabidhi Rahab,
“Nenda kafanye kazi yako kwa umakini”
Samson
alizungumza huku akijilaza pembeni ya Rahab, huku akijifungua vifungo
vya shati lake.Rahab akaichunguza moja ya bastola zake na kuikuta ikiwa
na risasi za kutosha, kwa haraka akajigeuza na kumkala tumboni Samson na
kumuweka bastola ya kichwa.
“Sema wewe ni nani?”
Rahab
alizungumza huku jasho jingi likimwagika, Samsona akamtazama kwa
umakini Rahab kisha akaunyanyua mkono wake wa kushoto pasipo kuwa na
waga na kuushika mkono wa Rahab alio shika bastola yake na kuusogeza
pembeni, mkono wa kulia wa Samson ukapakishika kiuno cha Rahab na
kumvuta chini taratibu na sura zao zikawa zimesogeleana kwa ukaribu sana
“Mimi ni fundi baiskeli”
Samson
alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa hisia nyingi za mapenzi, kisha
taratibu akaukutanisha mdomo waka nawa Rahab, na kuanza kubadilishaa
ladha ya mate yao, kila mmoja akajikuta mwili wake ukisisimka kwa kiasi
cha kuzidi kuziinua hisia zao za mapenzi huku kila mmoja akijitahidi
kumnyonya mwenzake vilivyo, wakaanza kuvuana nguo moja baada ya nyingine
na kujikuta wakizama katika dimbwi kubwa la mapenzi, huku kila mmoja
akionekana kuwa na furaha ya kupata penzi la mwenzake
Ndege
maalumu ya jeshi ikawekwa tayari kwa safari ya kuwasafirisha Fetty,
Halima, Anna na Agnes, ambao tangu wakamatwe maisha yao yamekuwa ni
yakufungwa vitambaa vyeusi machoni, huku mikononi na miguuni wakiwa
wamefungwa cheni nzzito ambazo si rahisi kwa wao kuweza
kuzifungua.Wakavalishwa mavazi ya rangi ya chungwa, yanayo endana na
mavazi ya mafundi gereji wengi.Safari ikapangwa kuondoka nchini usiku wa
saa nne
Waandishi
wa habar pamoja na wananchi wenye hasira kali na wasichana hawa,
wamejipanga pembezoni mwa barabara wakisubiria kuwaona wasichana hao
wakipelekwa katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari ya
kupelekwa mahakama kuu ya magaidi.Kila mmoja moyoni mwake akawa na sala
kubwa ya kuomba wahukumiwe kifungo cha maisha kwani ukatili ambao
wameufanya ni mkubwa, ambao haukuwahi kutokea katika nchi inayosifika
kwamba ni nchi ya amani.
Kikosi
maalumu cha wanajeshi wapatao ishirini na tano, wakiwa na bunduki zao
mikononi, wamesimama nje ya magari kumi aina ya GVC yanayotumiwa
kusafirishia wahalifu harari, Sifa ta magari haya ni kwamba hayaingii
risasi na yametengeneza kwa uwezo mkubwa wa kuhimiili mikiki mikiki ya
majambazi endapo wanaweza kuvamia msafara wao.Nitukio la kihistoria
nchini Tanzania kwani haijawahi kutokea ndio maana watu wengi pamoja na
waandishi wa habari wanaamu ya kushuhudia jinsi msafara huo utakavyokuwa
na ulinzi mkali kupita misafara yote ya magaidi walio wahi kukamatwa na
jeshi la polisi
Magari
yote kumi yakawa yapo tayari kwa safari, wanajeshi hao wakiwa
wanasubiria kuletwa kwa magaidi hao walio chini ya ulinzi mkali wa
askari.Simu ya IGP Bwana G.Nyangoi inata zikiwa zimesalia dakika tano tu
kabla hawajawafungulia magaidi kutoka kwenye chumba maalimu kilicho
tengenezwa kwa kuta za chuma, na kuwakabidhi katika kikosi maalumu cha
jeshi
“Ndio mkuu” Bwana Nyangoi alizungumza baada ya kuipokea simu yake
“Wahalifu , wabadilishieni msafara”
“Muheshimiwa mbona kila kitu tumeshakiweka kwenye utaratibu”
“Hii ni amri na sio ombi, wasafirisheni na sabmarine”
Rahab
na Samson, wakiwa wamevalia nguo za wahudumu wa ndege ya raisi aina ya
Air Force, wanafnikiwa kuingia katika ndege, pasipo kustukiwa huku
Samson akiwa ametengeneza vitambulisho bandia vinavyo endana na wahudumu
kwenye ndege ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Praygod
MakuyaMbaya zaidi katika siku hii, mtaalamu anaye kagua watu wanao
ingia kwenye ndege ya raisi kwa kutumia mashine maalumu, anaumwa sana
kiasi kwamba ameshindwa kuwemo katika ndege hii ya raisi, na watu
wengine hawana utaalamu wa kuitumia mashine hii kutoka ndege ni mpya
katika maisha yao.Samson katika mfuko wake wa nyuma wa suruali ameweka
kipakti kidogo chenye madawa ya kulevya yenye nguvu kubwa ya kumlewesha
mtu katika muda wa dakika tano tuu
Watu
wengi wamezoea kumuona Samson kama fundi baiskeli, na ndivyo jinsi watu
wengi wanavyo aminni katika hilo, ila sivyo kama watu wengi wanavyo
dhania.Samson ni miongoni mwa wapelelezi wa hatari kutoka nchini Somalia
katika kundi la Al-Shabab, Wazazi wake ambao kwa sasa ni marehemu ni
watanzania na ameishi Tanzani tangu akiwa mtoto mdogo na kupata elimu
yake ya msingi katika shule ya St. Mary, ila alipo timiza umri wa miaka
kumi na mbili aliwashuhudia wazizi wake, baba na mama wakiuwa kinyama na
Bwana Praygod Makuya ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri wa
mambo ya nje, wazazi wake walikuwa ni walikuwa ni miongoni mwa wanasiasa
mashuhuri nchini Tanzania kutoka katika chama pinzani, kinachokichua
chama kilichopo madarakani katika nafasi za kugombania madaraka ya
uraisi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )