Featured
Loading...

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 11 & 12

 

 MWANDISHI:EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA....
Anna akamuomba Rahab kuipokea simu hiyo
“Haloo”
“Dokta Will hapa nazungumza”
“Dokta vipi, mbona umetupiga na simu ya mezani?”
“Hilo halina tatizo sana, kikubwa nataka kuwaambi kuweni makini kwani kuna wanajeshi wametumwa kuja kuukagua huo msitu munapo ishi”
“Lini?”
“Unauliza lini? Wanakuja sasa hivi na wapo njia na hii taarifa nimepewa na kiongozi wao”

ENDELEA....
“Sawa nimekupata dokta”
“Cha kufanya ni kufunga handaki na nendeni mbali na lilipo”
“Hapa tulipo, ndio tulikuwa tunatoka, tunakwenda kuv......”
Fetty akamziba mdomo Rahab kabla hajaimalizia sentensi yake
“Mnakwenda wapi?”
“Kununua nguo za kuvaa”
“Sawa”
Rahab akakata simu

“Unajua wewe mtoto ni mwehu” Fetty alizungumza huku amemtolea macho Rahab
“Uwehu wangu upo wapi?”
“Unataka kumwambia kuwa tunataka kwenda kuvamia, hujui mazugumzo yote yanasikiwa kwenye mitandao ya simu”
“Ahaa, nilipitiwa”
“Sio kupitiwa, uacha hilo domo lako kubwa”
“Jamani hebu acheni kurumbana, ehee tuambie kuna ishu gani?”

“Anasema kuwa kuna wanajeshi wanakuja kuukagua huu msitu, na wapo njiani”
“Ahaaaa sasa inakuwaje?” Anna alizungumza
“Dokta amesema tufunge handaki na kuondoka, twende mbali na hapa”
“Mpango umeshakufaa huu” Halima alizungumza
“Sasa, mbona Ni shidaaaa” Agnes alizungumza huku akikaa kwenye kiti

“Jamani, tusiakate tamaa, kikubwa ni kuamua lile tunalo lihitaji” Fetty alizungumza
“Sawa, tunaamua je akili na maarifa yetu yanafikiria kile tunnacho taka kukifanya au tunaamua tuu, mwisho wa siku tufaye madudu ambayo yatatucost kwenye maisha yetu” Agnes alizungumza

“Nyinyi mbona waoga sana, kama maji tumeyavulia nguo tunapaswa kuyaoga” Rahab alizungumza
“Wewe acha misemo yako iliyopitwa na wakati, maji ukiyavulia nguo, ukiona yanazingua si unavaa na kuondoka.Kwani ni lazima kuoga” Anna alizungumza.

“Sikieni,dili limesha kufa kwa maana hapa kila mmoja anazungumza lake.Wapo wanao taka kufanya na wanao kataa.Sasa tuwafikirie hawa nguruwe wanao kuja huku”
 Fetty alizungumza huku akiwatazama wezake, hakuna aliye zungumza zaidi ya kufikiria cha kuzungumza.

“Watu wanasema, mwanaume hakimbii nyumba yake, bali anapambana kuhakikisha analinda mali zake na familia yake.Sisi sasa hivi ni sawa sawa na wanaume.Hapa ndio kwetu, hapa ndio tunapo ishi kwa amani.Hakuna aliyekuwa na kwake zaidi ya kutegemea maisha ya kuliwa na wanaume na kumnufaisha mwehu mmoja” Fetty alizungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo na msimamo

“Tunatakiwa kupambana, tunatakiwa kujilinda, Hatupaswi kukimbia makazi yetu.Kikubwa ni kuanyanyuka na kwenda kupambana na hao wanao jaribu kupambana na sisi.Hatuna uchaguzi mwingine.Simama lady’s”

Fetty alizungumza na kuwaamsha wezake walio kaa,wakazunguka duara moja na mikono yao ya kulia wakaikutanisha pamoja, huku wakiwa wamekunja ngumi.

“Tunatoka watano, tunarudi watano”  Agnes alizungumza
“KWA UMOJA TUNAWEZA”
Walizungumza kwa pamoja, kiasha wakaachiana, Kila mmoja akahakikisha silaha take ipo sawa
“Jamani ninapendekeza, tuvae vinasa sauti kwa ajili ya kuwasiliana kwa pamoja” Agnes alizungumza
“Hapo umenena wangu”

Anna alizungumza, akafungua kabati ambalo wameweka vinasa sauti, kila mmoja akachukua cha kwake na kukiweka kwenye masikio.Kila mmoja akahakikisha kinasa sauti chake kinafanya kazi

“Mnanisikia?” Halima alizungumza
“Ndio dada Halima” Rahab alijibu
“Fetty si ulivue hili jimwili” Agens alizungumza
“Nitapambana nalo hivyo hivyo”
“Mmmmm, haya big mama”

Wakacheka kwa pamoja na kutoka ndani ya pango,kila mmoja akaende njia yake huku wakiwa wameuzingira msitu wao.Kila mmoja akakaa kwenye nafasi ambayo angeweza kuona uingiaji wa wanajeshi hao waliotumwa kuja kufanya uchunguzi kwenye msitu.Kila mmoja akawa na hamu ya kutumia silaha yake, ambayo ameijaza risasi za kutosha.Masaa yakazidi kukatika pasipo kuona dalili yoyote ya majambazi kutokea kwenye msitu walio kuwepo.

“Jamani, mbona kimya? Agnes aliwauliza kupitia kinasa sauti chake
“Jua ndio linazama hivi” Rahbu alijibu
“Tuvuteni subira, kwa maana inaweza nao wamepanga kuvamia usiku” Fetty alizungumza
“Ahaa, jamani mimi njaa inaniuma” Anna alizungumza
“Wezako tunazungumza la maana wewe unazungumzia njaa hapa” Rahab alijibu

“Kwani kusema njaa, ndio nimekosea jamani?”
“Hujakosea ila ngoja tukamilishe hii kazi kwanza”
“Jamani kila mmoja awe makini kwenye pozi lake tunaumizana masikio” Halima alizungumza
“Powa bwana” Anna alizungumza
Masaa, yakazidi kukatika, hapakuwa na dalili yoyote ya mwanajeshi kutokea katika msitu wao.Hadi inatimu mida ya saa saa tano usiku hali ikaendela kuwa ya ukimya.

”Nimevumilia nimeshindwa, kama ni kuja waje tuu, Mimi ninakwenda kula jamani”
Anna alizungumza huku akisimama
“Hata mimi jamani” Rahab alizungumza
“Wewe si ulisema, tunazungumza ya maana subiri hao jamaa zako”
“Rahab na Anna tuachieni kelele” Agnes alizungumza
“Powa”

Anna akaanza safari ya kurudi lilipo handaki lao, hakuchukua muda sana akafanikiwa kufika kwenye handaki.Mazingira ya handaki akayakuta kama walivyo yaacha.Akafungua mfuniko wa handaki ambao ni wachuma na kushuka chini, huku bunduki yake ikiwa mkononi.Akawasha taa zote na kujirusha kwenye moja ya sofa huku akiwa amejichokea sana, Simu ya mezani ikamstua na taratibu akanyanyuka na kuifwata sehemu ilipo na akaipokea
“Hallo”
“Dokta Wille nazungumza”
 “Eheee”

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top