MWANDISHI : EDDAZARIA
ILIPOISHIA....
“Raisi……!!”
Rahab
alizungumza baada kwa mshangao baada ya kutokumuona Raisi Praygod
kwenye usawa wa bahari jambo lililoanza kumpa wasiwasi mwngi.Ikamlazimu
kurudi tena ndani ya maji, kutazama kama anaweza kumuona raisi, ila
hakumuuona
“Mungu wangu!!”
Rahabu
alizungumza kwa kuhamaki baada ya kuona kitu kikija kwa kasi katika
upande aliopo yeye, kwa haraka haraka akagundua kwamba ni samaki mmoja
hatari aina ya Papa, ndiye anaye karibia kufika katika eneo alilopo.
ENDELEA.....
Rahab
akaanza kujipapasa mwiki mwake kwa haraka, kwabahati nzuri akakikuta
kisu kwenye mguu wake wa kulika katika sehemu ya kiatu alipo kichomeka
kipindi alipokuwa akivaa, nguo alizo nazo kwenye chumba maalmumu cha
kuhifadhia nguo katika ndege ya raisi iliyo anguka muda mchache
uliopita.
Akajiweka
tayari kwa kupapambana na samaki huyu anaye mfwata kwa kasi katika eneo
ambalo ameangukia, kufumba na kufumbua samaki huyu tayari akawa
aweshafika katika eneo alipo Rahab, kwa ustadi wa hali ya juu Rahab
akajigeuza ndani ya maji na kushuka kwa kasi ndani ya maji, na
kusababisha samaki huyu mkubwa kupita juu yake, kwa kasi jambo lililo
zidisha ukali wa samaki huyu mwenye uchu wa kutafuna kiumbe chochote
kitakacho ingia kwenye enoa la bahari alipo yeye
Rahab
akakishika vizuri kishu chake chenye ncha kali, na kutazama jinsi
samaki huyu anavyo kunja kona na kurudi katika eneo alipo kwa kasi
kubwa, samaki akamfikia Rahab kwa karibu kabla samaki hajafanya maamuzi
ya aina yoyote, Rahab akamuwahi kumchoma kisu kwenye eneo la tumbo la
samaki huyu, lenye ngozi laini na kuanza kulichana kwa kutumia nguvu
nyingi, jambo lililo sababisa damu nyingi kutapakaa katika enoa la
sehemu walipo, huku utumbo mwingi wasamaki huyu ukitapakaa kwenye maji
“Haaaaaaaa”
Rahab
alizungumza huku akichomoza kichwa chake kwenye maji, huku akivuta
pumzi kwa wingi, akajilegeza mwili wake na kuufanya uanze kuelea elea
juu ya maji, huku akitazma juu mwili wake ukiwa umechoka sana
Agnes akamgeuza mtu aliye anguka na kumchunguza vizuri na kugundua
kwamba anamajeraha kadhaa kwenye mwili wake, Agnes akapiga mluzi ulio
mfikia Halima aliyekuwa katika eneo la karibu, Halima akapa hatua za
haraka hadi katika sehemu alipo simama Agnes
“Best kuna mtu hapa nimemuona”
Agnes
alizungumza huku akimgeuza mtu aliye lala chini huku damu zikimvuja,
Halima akamtazama mtu aliye lala chini kwa umakini, pasipo kuzungumza
kita cha aina yoyote, kiasha akaikoki bastola yake akiziweka risasi
zilizopo kwenye magazine yake, kuwa tayari kutoka nje, kitu kikubwa
alicho kibakisha ni kuivuta traiga ya bastola yeka kuziruhusu risasi
atakazo zihitaji kutoka nje
“Halima unataka kufanya nini?”
“Hastahili kuishi, mtu mwenye ni mfu huyu”
“Hembu ngoja kwanza?”
“Nini?”
“Usimuue?”
“Sasa anabaki duniani wa kazi gani, unamtambua huyu mtu”
Halima alizumgumza kwasauti iliyo jaa msisitizo mwingi
“Hata kama, simfahamu ila kuna kitu ninacho kihisi kwa huyu jamaa”
“Kwanza ametokea wapi?”
“Mimi sifahamu, ila nilisikia kishindo, nilipo kuja hapa ndipo nilipo muona huyu jaamaa akiwa amelala hapa”
Halima
pasipo kuuuliza akafyatua baadhi ya risasi, jambo lililo muudhi sana
Agnes na kumfanya amsukume Halima na kuangukia pembeni
“Mbona unakuwa mpumbavu wewe, nini unafanya”
Agnes
alizungumza kwa hasira huku akimfokea kwa nguvu Halima aliye angukia
pembeni, kwa bahati nzuri risasi alizo zifyatua Halima alizipiga pembeni
ulipo mwili wa jamaa na hapakuwa na risasi iliyo ingia katika mwili wa
mtu waliye muona.
Milio
ya risasi ikawastua Fetty pamoja Anna ikawalazimu kutoka nje ya
‘submarine’ na kuelekea sehemu walipo isikia milio ya risasi huku wakiwa
makini sana, kila mmoja akiwa ameishika bastola yake mkononi,
waakawakuta Agnes na Halima wakiwa wanafokeana huku kila mmoja
akionekana kuwa na jazba ya ajabu, Fetty akafyatua risasi mbili hewani
nakuwafanya Agnes na Halima kunyamaza
“Nyingi mumechanganyikiwa?”
Fetty aliuliza kwa sauti juu huku akiwatazama Halima na Agnes
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )