Rais
Robert Mugabe amekubali kung’atuka na kwamba ameshaandaa barua ya
kujiuzulu, shirika la utangazaji la CNN limeambiwa na chanzo
kilichokaribu na timu ya majadiliano upande mmoja wakiwemo majenerali
waliotwaa madaraka wiki iliyopita.
Chanzo
hicho kimedokeza kwamba majenerali wameridhia matakwa mengi ya Mugabe
ikiwa ni pamoja na kupewa kinga ya kutoshtakiwa yeye na mkewe Grace, na
abaki na mali zake.
CNN
limeambiwa kwamba chini ya makubaliano hayo, Mugabe na Grace
hawatashtakiwa. Pia, viongozi wawili waandamizi wa serikali ya Mugabe
waliliambia shirika la habari la Reuters Jumapili kwamba Mugabe alikuwa
amekubali kujiuzulu lakini hawakuwa wanajua yaliyomo katika mkataba wa
kuondoka kwake.
Ili ionekane amejiuzulu rasmi, utaratibu ni kwamba barua lazima iandikwe kwenda kwa Spika wa Bunge, chanzo kingine kimeongeza.
Mugabe
ambaye anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kila kona
aliwashangaza watu Jumapili alipokataa kufanya hivyo alipolihutubia
taifa kwa njia ya televisheni akiwa ikulu.
Chama
chake cha Zanu PF kimempa Mugabe, ambaye amekuwa katika kizuizi cha
nyumbani na jeshi lililotwaa madaraka kilimpa hadi jana mchana kuondoka
vinginevyo atashtakiwa bungeni.
Jumamosi, maelfu ya Wazimbabwe walijimwaga mitaani kupaza sauti zao wakimtaka mzee huyo mwenye umri wa miaka 93, ajiuzulu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )