Aliyekuwa
mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake
watano wamefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Ni
baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka
Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya
Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Hata
hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo
leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Katika
mashtaka hayo mawili ni ya kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya
ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa
kutendeka na kusababisha hasara.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na wapo nje kwa dhamana
baada ya kukamilisha masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili
wanaominika, kila mdhamini akisaini bondi ya Sh 12 milioni.
Pia washtakiwa hao watoe fedha taslimu Sh 12 milioni ama mali isiyo hamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )