Watu
hao waliwekewa alama za X wakitakiwa kubomoa kwa hiari yao Novemba 25
mwaka jana kwa mara ya mwisho wakitakiwa kupisha eneo la hifadhi ya
reli walilovamia.
Akizungumza
jana Desemba 3 mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, Ofisa Uhusiano wa
kampuni hiyo, Catherine Moshi alisema bomoabomoa hiyo ilihusisha
vibanda vya stendi ya daladala ya Jamatini, vibanda vya stendi ya mabasi
ya kwenda mikoani, Ofisi za kampuni ya mabasi ya Shabiby na Abc,
Mgahawa wa Cape Town na kituo kimoja cha mafuta kilichokuwa karibu na
ofisi za Shabiby.
Kuhusu
stendi ya mabasi, amesema wamekubaliana na uongozi wa mkoa na manispaa
kuwapa muda wa kuondoa stendi mbili za mabasi yaendayo mkoani na ya
daladala ya Jamatini.
“Wamesema
kuondoa stendi sasa italeta shida kwa hiyo kuna makubaliano ambayo
tumekubaliana na Mkuu wa Mkoa (Dk Binilith Mahenge) wa kutoa muda wa wao
kuzihamisha,”alisema.
Hata
hivyo, alisema makubaliano yao si kwamba stendi hizo zinabaki bila
kubomolewa bali ni kwa muda na ukiisha wawe wamepata eneo la kupeleka
huduma hizo ili eneo libaki tupu likabidhiwe kwa mkandarasi.
Alisema
wamemaliza kazi hiyo kwa Dodoma mjini isipokuwa maeneo ya kanisa,
misikiti, makaburi na ambayo mahakama imezuia ikiwemo kituo cha mafuta
kilichomo mkabala na stendi ya daladala ya Jamatini.
Moshi
amesema wamebomoa nyumba kamili 128 na vibanda 487 ambazo waliziwekea
alama lakini wapo wengine walioamua kujiondoa wenyewe.
Amesema
kuwa walishasaini mkataba na mkandarasi Novemba 29 mwaka huu na kwamba
kabla ya kumkabidhi mkandarasi eneo hilo ni lazima wahakikishe kuwa
njia ya reli ziwe safi.
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara hao, John Banda alisema kuwa makubaliano na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge yaliyofanyika Ijumaa hayakutekelezwa
baada ya kufika katika eneo hilo Jumamosi akiwataka wafanyabiashara hao
kuondoka.
Awali
wafanyabiashara hao waliomba kupewa muda wa kuhama na kuonyesha eneo
jingine la kufanyia biashara baada ya kuondolewa katika eneo hilo.
“Jumamosi
Mkuu wa mkoa alifika katika eneo hilo kuwapelekea wafanyabiashara
majibu aliyoyapata baada ya kukutana na kamati yake ya ulinzi na
usalama. Aliwaambia watu wa Jamatini ni vyema kila mmoja aondoe kibanda
chake yeye mwenyewe,” amesema.
Amesema
kuwa amekwenda kule (kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa) amepata
elimu. Amekuja kuwaletea majibu ya kamati ya ulinzi na usalama kuwa ni
vizuri kubomoa wenyewe kabla ya kusubiri kuondolewa.
Amesema
kuwa eneo walilopelekwa la Makole lilopo nyuma ya mahakama halina
biashara kwa sababu wateja wao wakuu walikuwa wakiwategemea ni abiria
wanaotumia stendi hizo.
“Eneo
hilo (Makole) lina vumbi sawa lina miundombinu ya vyoo na nini. Lakini
kikubwa kule hakuna biashara kwa sababu wateja wetu ni abiria,” amesema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )