Makamu
wa Rais, Samia Suluhu leo Ijumaa Desemba 15 amehamia rasmi makao makuu
ya nchi ikiwa ni mwendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia
Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo
"Nilikuwa
hapa kwa muda mrefu kidogo lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba
15 na nimefurahi kwamba nitafanya kazi mahala pangu pa kazi pa kudumu,"
amesema Samia.
Amesema
kauli mbiu yake kwa wakazi wa Dodoma ni kuufanya mji huo kuwa wa kijani
hivyo Desemba 21 ataendesha mpango wa kupanda miti katika wilaya zote.
"Kwa kuwa nasimamia pia masuala ya mazingira nitaendesha zoezi hilo ili kurudisha hali ya Dodoma," ameongeza.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )