RAIS
John Magufuli amesema Serikali imebaini kuwa kampuni ya Mawasiliano ya
Bharti Airtel ni mali ya Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL) na
amemwagiza Waziri wa fedha na mipango kufuatilia suala hilo haraka ili
Airtel irudishwe kumilikiwa na serikali.
Rais ameyasema hayo leo Desemba 20 wakati akizungumza kwenye Ofisi za Taifa za Takwimu mjini Dodoma.
“Kampuni ya AIRTEL imethibitika kuwa ni mali ya Shirika la TTCL, lakini kuna mchezo ulifanyika, sasa sitaki kuongea sana. Nataka Waziri wa Fedha ufuatilie suala hili kabla ya mwaka huu kuisha,” amesema Magufuli.
Rais ameyasema hayo leo Desemba 20 wakati akizungumza kwenye Ofisi za Taifa za Takwimu mjini Dodoma.
“Kampuni ya AIRTEL imethibitika kuwa ni mali ya Shirika la TTCL, lakini kuna mchezo ulifanyika, sasa sitaki kuongea sana. Nataka Waziri wa Fedha ufuatilie suala hili kabla ya mwaka huu kuisha,” amesema Magufuli.
Taarifa
na ndani zinabainisha kwamba hisa za Airtel zinatarajiwa kukabidhiwa
kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuendesha biashara za
kampuni hiyo yenye wateja wengi zaidi nchini ikiwa nyuma ya Vodacom na
Tigo.
Chanzo
cha mpango huo kinatajwa kuwa ni uongozi wa juu wa TTCL uliotaka
Serikali kudai haki zake za uwekezaji ndani ya Airtel ambako inaimiliki
kwa ubia wa asilimia 40 kwa 60 na mwekezaji.
Taarifa
zinaarifu kuwa TTCL itamiliki hisa zote za Airtel Tanzania Limited
ambapo tayari TTCL imewasilisha hoja ya kutaka kufanya hivyo baada ya
kubaini kwamba Serikali ilipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji.
Hoja
ya TTCL inaanzia Novemba 3, 1998 ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet
ambayo ilifanya kazi mpaka Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa
Celtel Tanzania huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya shirika hilo
kwa asilimia zote baada ya kuwekeza Dola milioni tano za Marekani (zaidi
ya Sh11 bilioni sasa).
Lakini,
Januari 31, 2002, Celtel ikiwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa kiasi
cha Dola 82 milioni (zaidi ya Sh180.4 bilioni) ili kukuza mtaji wake.
Kwa
kipindi hicho, TTCL iliyokuwa na thamani ya Dola 600 milioni (zaidi ya
Sh1.32 trilioni) ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na
Kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi. Serikali
ilikuwa inamiliki asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35
zilizosalia.
Agosti
5, 2005, mabadiliko yalifanywa kwenye bodi ya wakurugenzi wa Celtel kwa
lengo la kuunda kampuni mbili tofauti; Celtel ikitenganishwa na TTCL.
Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI
ambayo Septemba 2007 iliuza hisa zake kwa Zain ambayo nayo ilikuja
kuziuza kwa Bharti Airtel, Juni 8, 2010.
Imeelezwa
kuwa TTCL inadai uwekezaji wake ilioufanya Celtel baadaye Airtel ambayo
thamani yake imeongezeka maradufu sasa haulingani na inachokipata hivyo
kutaka kusimamia biashara za kampuni hiyo ya mawasiliano.
Hoja
ya madai hayo ni namna umiliki wa hisa ulivyobadilishwa baada ya Celtel
kutenganishwa na TTCL ambayo ilipewa hisa chache tofauti na
ilivyostahili.
Kwa
sasa, Airtel Tanzania inamilikiwa na Serikali yenye asilimia 40 na
Celtel Tanzania BV, kampuni tanzu ya Zain Africa BV ambayo ilinunuliwa
na Bharti Airtel International, Novemba, 2010 ikiwa na asilimia 60.
Katika
mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, Serikali iliilipa Bharti Airtel
Sh14.7 bilioni hivyo kuchukua asilimia 35 ya hisa ilizokuwa inamiliki na
kuifanya imiliki asilimia zote za TTCL.
Sheria
mpya iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge imeibadili TTCL inayohudumia
asilimia 0.82 ya soko kuwa shirika la umma la mawasiliano na kulipa
jukumu kubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.
Bharti
Airtel inatakiwa kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la
Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kukidhi vigezo vya sheria ya posta na
mawasiliano ya mwaka 2010, lakini bado haijafanya hivyo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )