Featured
Loading...

APATOSHI CHAMA KIPYA CHA ACT...!!! Tetesi Mwenyekiti Taifa Atishia Kuachia Ngazi



By G Sam -JF
Mgogoro wa kimajukumu umeanza kuibuka ndani ya chama kipya cha ACT-Wazalendo ambapo mwenyekiti wa taifa wa chama hicho bi Anastazia Mghwira jana alitishia kuachia ngazi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinadai kuwa kiongozi mkuu wa chama Kabwe @ Zitto alimuonya mwenyekiti huyo kuwa anaingilia majukumu ya kukieneza chama ambayo kimsingi si yake.

Kwa mujibu wa katiba ya ACT-Wazalendo, kazi ya kukieneza chama ni ya kiongozi mkuu ambapo mwenyekiti kazi yake ni kuongoza vikao vya chama na kusimamia maadili ya wanachama.

Kufuatia mgogoro huo mwenyekiti huyo alitishia kujiondoa ndani ya uongozi wa chama hicho kutokana na mkanganyiko wa kimajukumu kati ya mwenyekiti na kiongozi mkuu.


My take!
Muda si mrefu Zitto atajihalalishia uenyekiti wake ndani ya ACT ambao umo chini ya kivuli cha Anastazia Mghwira na kuitimiza rasmi azma yake ya muda mrefu!

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top