EDWARD Lowassa, mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti Yusuf Aboud … (endelea).
Lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama
sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza
kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.
“Ni kweli chama chetu kimemshindwa
Lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa Lowassa
yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,”
anaeleza mjumbe mmoja wa NEC aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa Mtandaoni.
Amesema, “Kwa maoni yangu, hatua hii
itakidhoofisha zaidi CCM kuliko kukiimarisha. Kama CCM inajitakia mema,
hakiwezi kuruhusu Lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu.
Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”
Jumatatu, Kamati ya Maadili ya chama
hicho iliyodai ilikuwa na “faili la Lowassa na watuhumiwa wengine sita,”
imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari
imemalizika.”
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa
ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru Lowassa” kunathibitisha udhaifu
wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.
Taarifa zinasema, ikiwa Lowassa
atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea
kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na
matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.
Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya
Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack
Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai
ya matumizi mabaya ya madaraka.
Wengine wanaoweza kufikishwa
mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao
watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.
Jakaya Kikwete ambaye ndiye rais wa
Jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “Lowassa
hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”
Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara
moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa Lowassa anaungwa mkono katika mbio zake
za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rostam ametajwa
kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Col. Apson
Mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya Lowassa.”
Rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za
biashara zake nchini Kenya na Dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa
Kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.
Mfanyabiashara huyo ambaye amewahi
kuwa mbunge wa Igunga (CCM), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi CCM na
kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya
kwanza ya utawala wa Kikwete, Rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.
Mbali na Rostam Aziz, Lowassa
amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii,
akiwamo Andrew Chenge na Nazir KaramagiTupe Maoni Yako( Matusi Hapana )