Majenerali watatu waliojaribu kufanya
jaribio la mapinduzi nchini Burundi wamekamatwa, lakini kiongozi wao
aliyeongoza jaribio hilo la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza bado “yuko
mafichoni".
Baada ya makabiliano makali ya udhibiti
wa makao makuu ya redio na televisheni ya taifa kushuhudiwa jana,
barabara za mji mkuu Bujumbura zimebaki kuwa tulivu hii leo.
Rais Nkurunziza ambaye alirejea jana
nchini humo kutokea Tanzania, ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa
viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati jaribio la mapinduzi
likiendelea nchini mwake, anatarajiwa kulihutubia taifa wakati wowote
kuanzia hivi sasa.
Msemaji wa rais Gervais Abayeho amesema
Jenerali mmoja wa poli na majenerali wawili wa jeshi walikaamtwa kwa
kuhusika katika mapinduzi hayo yaliyoshindwa.
Ameongeza kuwa mmoja wao alikuwa Waziri wa zamani wa Ulinzi Cyrille Ndayirukiye.
Lakini kiongozi wa mapinduzi hayo
Goedfrpid Niyombare ambaye alitimuliwa na Nkurunziza kama mkuu wa
ujasusi, hajakamatwa maana hajulikani aliko.
Jenerali Niyombare ameliambia shirika la
habari la AFP kwa njia ya simu kuwa anataka kujisamilisha, akitaraji
kuwa hawatauliwa na vikosi vya serikali.
Jaribio hilo la mapinduzi linafuatia
wiki mbili za maandamano mjini Bujumbura, ambayo waandamanaji kila mara
walipambana na polisi, ambao walionekena wakiwafyatulia risasi za moto.
Zaidi ya watu 20 waliuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Msemaji wa kundi lililoongoza mapinduzi,
Zenon Ndabaneze, amezungumza na AFP akithibitisha kuwa wanamapinduzi
waliamua kujisalimisha baada ya kukamatwa na polisi.
Afisa mmoja wa polisi amesema wamewaweka kizuizini wanajeshi hao waasi ili wawafungulie mashtaka.
Kundi moja la mashirika ya kiraia ambalo
liliongoza maandamano hayo ya kumpinga rais Nkurunziza limetoa wit oleo
wa kuendelea maandamanao.
Gordien Niyungeko naibu kiongozi wa
Focode, mojawapo ya mashirika ya kiraia 300 yaliyoandamana, amesema
manaandamano yao yataendelea maana kundi lake halihusiki kwa vyovyote
vile na jaribio lililoshindwa la mapinduzi.
Kundi moja la vijana katika kitongoji
cha Cibitoke, cha mji mkuu Bujumbura, eneo ambalo lilikuwa kitovu cha
maandamano, limesema wameonywa na polisi kuwa watachukuliwa kuwa wao ni
waasi na watafyatuliwa risasi ikiwa wataandamana.
Nayo Marekani imewaonya raia wake
kutokwenda nchini humo na kuwataka wale walioko kule kuondoka haraka
iwezekanavyo. Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Kigeni imesema Burundi
inakabiliwa na hali mbaya ya usalama.
Imesema kundi la kigaidi la Al-Shabaab
limetishia kufanya mashambulizi nchini Burundi na pia huenda likawalenga
raia wa Marekani.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri:Josephat Charo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )