Musa Mateja
Mjengo anaoishi mkali wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba uliopo Kunduchi-Mbezi Beach jijini Dar, unadaiwa kuzua utata mkubwa hivyo kulilazimu Risasi Jumamosi kuchimba na kubaini kuwa nyumba hiyo si ya msanii huyo bali amepangisha.
Mjengo anaoishi mkali wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba uliopo Kunduchi-Mbezi Beach jijini Dar, unadaiwa kuzua utata mkubwa hivyo kulilazimu Risasi Jumamosi kuchimba na kubaini kuwa nyumba hiyo si ya msanii huyo bali amepangisha.
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
Awali, Kiba alikaririwa akisema kuwa,
mjengo huo wa kifahari ni wa ndugu yake aliyepo nje ya nchi ambaye
alimpa ili aishi na ndugu zake (wa Kiba) wakati yeye (mmiliki) akiwa
hayupo.Siku kadhaa mbele, baada ya Kiba kuvamiwa nyumbani hapo na watu
kupora vitu huku akinusurika kuuawa, jamaa huyo alikaririwa redioni na
kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa nyumba hiyo ni yake.
Ilidaiwa kwamba, mara tu baada ya Kiba
kutangaza kumiliki nyumba hiyo, ilidaiwa kuwa aliibuka mwanamke
aliyetajwa kwa jina moja la Mariana ikisemekana eti ndiye mmiliki halali
wa nyumba hiyo.Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba, Mariana,
akiwa mwandani wa Kiba ndiye aliyemuweka Kiba aishi kwenye nyumba hiyo
wakati yeye (Mariana) kwa sasa anaishi nchini Singapore barani Asia.
“Ninyi mnasema ule mjengo ni wa Ali
(Kiba)? Acheni hizo, kwa taarifa yenu hiyo nyumba kapewa na mrembo
f’lani hivi amazing, anaitwa Mariana, ni Mbongo anayeishi Singapore.
“Muulizeni huyo Kiba awaambie ukweli,”
kilisema chanzo chetu kikisisitiza: “Hata Mariana aliposikia eti nyumba
ni ya Ali (Kiba) alishangaa na akamaindi ile mbaya hivyo kwa sasa
sidhani kama wanaelewana kwa ajili hiyo.”
Baada ya kukutana na mkanganyiko huo,
gazeti hili lilimtafuta Kiba ambaye alikiri kwamba kweli nyumba hiyo
siyo yake bali amepangisha huku akikana kusema kuwa
anaimiliki.Alipoulizwa juu ya madai ya kupewa nyumba hiyo na mwanamke
aitwaye Mariana, Kiba alisema hayo ni maneno tu kwani anachojua yeye
amepangisha.
“Kwanza hebu nitumie picha nijue ni nyumba gani?” aliomba Kiba ambapo alitumiwa picha kwa WhatsApp ndipo akajibu:
“Okey, kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba.”
“Okey, kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )