BAADA
ya wiki kadhaa kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni
likiwa limevuka nakuachia ‘nido’ wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akipiga
stori na Over The Weekend, Shilole alisema kuwa anajua kwamba kitendo
hicho kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile.
“Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili
halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,”
alisema. Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji
kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )