Moja
kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ni mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo
yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha
operesheni hiyo ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti
wa CCM, Jakaya Kikwete amesema kuwa ataachia nafasi hiyo hivi karibuni
na kumkabidhi Rais Magufuli, lakini alitoa angalizo kuhusu uhusika wake
kwenye chama hicho baada ya kujivua kofia hiyo nzito.
Ingawa
Katiba ya Chama hicho inaeleza kuwa mwenyekiti mpya atapatikana mwaka
2017, Mwenyekiti wa Chamo hicho, Dk. Jakaya Kikwete amepanga kuachia
nafasi hiyo mapema (mwaka huu) kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.
Akiongea
jana kwenye uzinduzi wa Kitabu cha maisha ya kada maarufu wa chama
hicho, Marehemu Captain John Komba, Dk. Kikwete alieleza kuwa ataachia
nafasi hiyo lakini hataacha kushiriki vikao vya ndani na mambo ya
maamuzi ya chama hicho.
“Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nitaachia, lakini mambo ya ndani yanayohusu chama hiki sitaacha kushiriki,” alisema.
Februari
mwaka huu, Dk. Kikwete aliwaambia wazee wa CCM mjini Singida kuwa
sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa chama hicho mwaka huu, zilikuwa
sherehe zake za mwisho akiwa kama Mwenyekiti.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )