Waasi wanaompinga Rais Pierre Nkurunziza wameungana kuunda vuguvugu moja
linalofahamika kama The Republican Force of Burundi, na limetangaza
vita dhidi ya kiongozi huyo.
Kubuniwa kwa vuguvugu hilo kunatukia huku shinikizo kutoka kwa mataifa ya kanda hiyo, zikiongezeka.
Umoja wa Afrika unaitaka serikali ya Nkurunziza ikubalie walinda amani wa Umoja wa Afrika.
Hata hivyo serikali yake imekatalia mbali ombi hilo ikidai kuwa, haiko
katika hali ya mapigano yawenyewe kwa wenyewe wala hakuna hatari ya
kuibuka kwa mauaji ya kimbari kwa hivyo inaichukulia jeshi hilo la
kulinda amani kama jeshi la kigeni na "kikosi cha uvamizi".
Umoja wa Afrika unaitaka serikali ya Nkurunziza ikubalie walinda amani wa Umoja wa Afrika.
Tanzania imejitokeza kupinga mpango huo wa AU wa kuwatuma wanajeshi elfu
tano, wa kulinda amani wanaopangiwa kwenda Burundi, kusaidia kukomesha
ghasia na umwagikaji zaidi wa damu.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga, yuko
katika ziara ya kidiplomasia nchini Uganda na kisha Burundi kuhusiana na
mzozo huo katika taifa hilomojawepo ya kanda ya Afrika Mashariki.
Rais wa Uganda anatarajiwa kuongoza mchakato wa amani kuanzia jumatatu
Msemaji wa serikali ya Burundi Willy Nyamitwe amenukuliwa na shirika la
habari la AFP akisema kuwa hofu ya kuibuka kwa kundi lipya la waasi sio
tishio katika serikali ya Burundi.
Nyamitwe anasema kuwa Republican Forces of Burundi, ama "Forebu" haitadumu.
''sio mara ya kwanza kwa makundi ya waasi kuibuka hapa Burundi. Tutawakanyaga mara moja''
Nyamitwe anasema kuwa Burundi ina haki ya kimsingi ya kulinda maisha na
usalama wa wananchi wake na kuwa haitachelewa kuwazima mara moja.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )