Uchaguzi
Mkuu ulifanyika tarehe 25.10.2015 na wananchi wa Jiji la DSM Waliamua
kuongozwa na UKAWA na ndio maana walichagua Madiwani na Wabunge wengi
kutoka UKAWA. Kati ya Majimbo 10 ya Uchaguzi katika Jiji la DSM CCM
ilipata Majimbo 3 tu baada ya kuchakachua na UKAWA ilipata yaliyosalia.
Hali
ni hiyo hiyo kwenye kata. Wananchi waliamua kuipumzisha CCM kwa kuwa
walikua wamechoshwa na uendeshaji mbaya wa Jiji la Dar es Salaam . Tangu
Uchaguzi umalizike mpaka leo wananchi wanakosa huduma za Jiji kwa
sababu CCM ilitaka kushinda Umeya wa Jiji kwa staili ileile waliyozoea
ya goli la mkono.
Mara
wakaletwa wapiga kura feki kutoka Zanzibar huku Wakijua wazi kuwa
TAMISEMI sio jambo la Muungano. Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI
hajawahi kutoa kauli wala kukemea hali hiyo hata siku moja huku akijua
wazi kuwa vitendo hivyo vilikua ni kinyume Cha sheria za Nchi.
Leo
tarehe 27.02.2016 tumeshuhudia Uchaguzi ukiitishwa na baada ya wajumbe
Kuwasili wakakutana na kilichoitwa zuio la Mahakama la Tangu tarehe
05.02.2016 .
Jambo
hili limetokea baada ya Taarifa kusambaa jana tarehe 26.02.2016 kuwa
CCM walipeleka shauri mahakamani la kuweka zuio na kuwa shauri hilo
lilitupiliwa Mbali.
Nini
kinafichwa Jiji la DSM ? Tuna taarifa kuwa ni Ufisadi mkubwa uliofanywa
na viongozi wa Jiji waliopita na wakishirikiana na Viongozi wa CCM
kupora Mali za Jiji kama vile UDA, Mali za soko la Kariakoo, Viwanja na
majengo ya Jiji.
Pili
tuna Taarifa kuwa hawataki majipu ya Jiji yatumbuliwe kwani kuna vigogo
wakubwa wa CCM watatumbuliwa kutokana na kushiriki kwenye Ufisadi
mkubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam . Mipango iliyopo.
Mkutano
wa Uchaguzi Leo uliitishwa pamoja na kuwepo hicho kinachoitwa zuio la
Mahakama kwa lengo la kuwaudhi Madiwani wa UKAWA ili waonekane kuwa
wanafanya fujo .
Hii
ni kutokana na ukweli kuwa kama zuio lipo Tangu siku CCM wanaadhimisha
miaka39 ya kuzaliwa kwake ni kwanini Mkurugenzi aliitisha mkutano wakati
akijua Mahakama imeweka zuio?.
Mpango
huu umesukwa ili kuhakikisha kuwa Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI
anatengenezewa sababu za kuweza kuvunja Halimashauri ya Jiji la Dar es
Salaam na kuunda Tume ya kuongoza Jiji.
Ni
vyema tukaweka angalizo mapema kuwa Mafisadi wana mikakati mingi sana
ya kuhakikisha kuwa hawatumbuliwi Majipu. Kama Rais ambaye ndio Waziri
mwenye dhamana na TAMISEMI hakubaliani na mbinu hizi za Mafisadi,
aingilie Kati Mara moja na kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa Meya unafanyika
na kazi ya kutumbua majipu ya Jiji inaendelea kama ambavyo imeshaanza
katika Manispaa za Ilala na Kinondoni zinazoongozwa na UKAWA .
Imetolewa na John Mrema.
Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri CHADEMA.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
