Featured
Loading...

Baada ya Chama Cha Walimu Kukosoa Mpango wa ‘Daladala za Bure Kwa Walimu’ Dc Makonda Kawajibu Hapa

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Jumapili ya February 28 2016 alitangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam wataanza kupanda daladala bure kuanzia March 7 2016 baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, habari hii wengine wakaipokea vizuri wengine wakaikosoa.

Dc Makonda amehojiwa na millardayo.com na kusema ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi , watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa‘

‘Huu ni mchango wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja tu na inabidi watu wajue huu sio mpango wa serikali, ni wadau wamekubali kusaidia Walimu, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa‘ – Makonda
‘Nadhani Walimu walitakiwa kwanza kushukuru wamekumbukwa, ningefurahi wangesema tumepokea nafasi ambayo jamii sasa imeanza kutambua heshima ya Walimu, kwa moyo huu ambao Wadau wameuonyesha tunaiomba sasa wizara ya elimu iendelee kuangalia kuboresha zaidi‘ DC Makonda

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top