Kumekuwa na minong’ono mingi kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu Filamu
ya Mapenzi ya Mungu ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo
ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos Nchini
Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA).
Ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa
kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika
mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya
Munguni Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani
anahaki zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo.
Filamu ya Mapenzi ya Mungu imetengenezwa chini ya kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.
IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )