Featured
Loading...

Breaking News: Timu ya Taifa ya Chad Yajitoa Katika Mashindano ya AFCON



Timu ya taifa ya chad imejitoa katika mashindano ya kugombania nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya mataifa ya Africa itakayo pigwa Gabon

Chad imeshindwa kufika Jjini Dar es salaam kwa kile walicho eleza kuwa  nchi yao imeyumba kiuchumi kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani kuikumba nchi hiyo

Hivyo mchezo wake na Taifa Stars uliopangwa kufanyika kesho hautokuwepo na kwa mujibu wa sheria  ya Tanzania, huenda Taifa Stars itapewa mogoli 2 na alama tatu hivyo kufikisha alama 7 kujitoa kwa chadi kuna liweka kundi G liwe gumu sana

“Timu yetu haiwezi kusafiru hadi Dar es salaam kwa mechi ya tarehe 28, nchi yetu imeathirika na mgogoro wa uchumi duniani,hivyo ushiriki wetu kwenye mashindano mbali mbali umepata pigo kubwa kutokana na ukosefu wa fedha, tunaomba radhi kwa usumbufu” 
Taarifa  ya chama cha soka nchini Chad imeeleza. Taarifa hii imeripotiwa na mtandao wa Supersports.com mapema leo

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top