Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Jenister Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe
uliotangazwa leo Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa usiku huu imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa
kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu, uteuzi mpya kwa mujibu
wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa zitatolewa kwa wananchi