Featured
Loading...

Rais John Magufuli Awashukia Umoja wa Afrika Mashariki Kuhusu Gharama za Mikutano ndani ya Hotel ya Ngurudoto Badala ya AICC

Wakati Rais Magufuli anatoa hotuba ya kufunga mkutano wa Afrika mashariki, uliofanyika ndani ya ukumbi wa Ngurdoto, alitema cheche zake na kuwapa picha halisi watu wa afrika mashariki, kuhusiana na ubanaji wa matumizi.

Rais anashangaa kwanini mikutano ya afrika ya mashariki ifanyike kwenye hoteli ya Ngurdoto wakati kuna ukumbi wa AICC ambao hauna gharama kama zinazotozwa na hoteli ya hadhi ya Ngurdoto. Rais Kenyatta aliinamisha kichwa huku akicheka, wajumbe wote kwenye ukumbi wakauelewa ujumbe wa ubanaji wa matumizi.

Lakini ni Ngurdoto hii hii ambayo wakati awamu ya nne inaanza kazi, ilihodhi semina elekezi, ambayo ilitumia fedha nyingi. Sina uhakika, nadhani kwamba mmiliki wa hii hoteli atakuwa ni mmoja wa vigogo wa nchi hii, hivyo tenda za uhakika kama vile semina elekezi na mikutano ya east africa, huwa ni kipindi cha neema.

Sekretarieti ya east african community imekumbushwa kuwa watu wa ukanda huu ni masikini, hivyo wasipende anasa za ajabu ajabu. Ni ujumbe mzuri, ila mmiliki wa hoteli ya Ngurdoto atauchukia sana uongozi mpya wa Rais Magufuli ndani ya jumuia ya afrika ya mashariki, katangaziwa njaa tangu mapema kabisa.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top