Aidha Baraka amekiri kuwa na mtoto na anajivunia kiasi kwamba hawezi kukaa bila kutuma matumizi ya mtoto kama inavyodaiwa.Baraka ameweka wazi kuwa mama yake na ndugu zake wanaweza kuwa shahidi ni jinsi gani anamuhudumia mtoto huyo na ana mihamala ya simu inayoonyesha pesa alizotuma kwa mama mtoto wake.
Baraka amesema kuwa hana uhakika kama aliyetoa taarifa hizo ni mama wa mtoto wake kwani kwa anavyomjua sio mtu wa kuongea sana na amejaribu kumpiga simu hakupokea.
Pia Baraka kama mama wa mtoto wake ameamua kufanya hivyo itakuwa ni hila zake tu za kumchafua kwa kuwa labda walishaachana na anaona kuwa yuko na mtu mwingine na yeye ni staa na kuongeza kuwa zaidi ya kuzaa mtoto hawana mahusiano yoyote.
Baraka ameweka wazi pia hii ndiyo taarifa namba moja iliwahi kum dissapoint na kumuumiza kwa kuwa yeye anajua anajua ni jini gani anampenda mwanae halafu watu wanasema vingine.
Pia Baraka da Prince ameeleza kuwa aliwahi kumuona mtoto huyo alipokwenda Iringa kwenye show kwani hakuwa amewahi kumwona toka amezaliwa akaona ni vyema kumwona.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )