Takwimu zinatajwa kuwa Yanga na Azam FC kabla ya mchezo wa leo wamekutana jumla ya michezo 15 kila timu ikiwa imeshinda mara tano na kutoka sare mara tano. Katika mchezo wa leo March 4 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Yanga na Azam FC zimemaliza mchezo huo kwa sare ya goli 2-2.
Azam FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 11, baada ya beki wa Yanga Juma Abdul kujifunga na baadae kusawazisha goli hilo dakika ya 28, Yanga waliongeza kasi baada ya kusawazisha na dakika ya 41 Donald Ngoma akapachika goli la pili.
Kwa upande wa Azam FC wao walisawazisha goli lao dakika ya 70, kupitia kwa nahodha wao John Bocco ambaye ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli ya kuifunga Yanga wakutanapo dhidi ya Azam FC, kwani hilo lilikuwa goli la nane kwa Bocco kuifunga Yanga.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )