Machi
15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe
Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo
mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu
kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.
Agizo
hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali
watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa,
kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli
za uzalishaji mali.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake
hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.
CCM
inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha
kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye
kuwa Rais wa Serikali
ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
CCM
kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake
inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya
kumpongeza kwa kuanza
vizuri
katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi
hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila
ngazi.
Historia
ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa
Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu
ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya
Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila
mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.
Utekelezaji
wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha
uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa,
ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na
ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.
Matokeo
hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo
yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na
umaskini kwa
ustawi wa jamii kwa ujumla.
Aidha
CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na
serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa
umma.
Kumbukumbu
zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni
pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma
mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo
vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi
ya utawala bora.
Hata
hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa
Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta
na uonevu.
Naomba
ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya
uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji
katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na
serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa
ya watanzania walio wengi.
Watanzania
walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na
uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri
hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo
yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo
ambalo CCM haikubaliani nalo.
CCM
inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania
wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais
Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye
Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.
………………………………………………………………………
Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
20/03/2016
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )