Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo moja,
akiwamo anayedaiwa kuwa kigogo wa biashara ya dawa hizo nchini.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa, juzi saa 1.15 usiku katika maeneo ya Mbezi Beach,
walimkamata mtuhumiwa wa kwanza akiwa na gari baada ya kumpekua alikutwa
na dawa hizo za kulevya.
Alisema
walipomhoji zaidi, alidai kuwa dawa hizo siyo zake, bali za tajiri yake
anayeishi Mikocheni jijini hapa ambaye wali panga kukutana naye maeneo
ya Mbezi Beach kwa ajili ya kukabidhiana.
Alisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Kukamatwa
kwa kigogo huyo na msaidizi wake ni mafanikio ya jeshi hilo ambalo hivi
karibuni lilimkamata kigogo mwingine muuza ‘unga’ jijini hapa hivi
karibuni.
Wakati
huohuo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo
chake cha usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya
usalama barabarani
Jumla
ya Tshs. 577,831,000 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa
mida wa siku 12, kuanzia 07/03/2016 hadi tarehe 18/03.2016.
Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.
Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )