Mayasa mariwata, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Staa wa filamu Bongo,
Elizabeth Michael ameendelea kuzua minong’ono kutokana na kitendo cha
kutoshiriki kwenye mikusanyiko ya wasanii wenzake hadi kufikia hatua ya
kutengwa.
Hali hiyo ya sintofahamu ilijidhirisha
Jumanne iliyopita kwenye hafla ya kumpongeza Paul Makonda kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na wasanii wa Bongo Muvi chini ya
uratibu wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ katika Hoteli ya Rodizio
iliyopo Masaki, jijini Dar.
“Jamani! Mbona Lulu hajifunzi kutokana
na makosa? Juzi alipokuwa akirudi na tuzo kutoka Nigeria, hatukwenda
kumpokea kutokana na yeye kutokupenda kujumuika na wasanii wenzake,
angalia sasa, hata leo hajaja kama kawaida yake.
“Nilidhani atabadilika kumbe wapi.
Anapaswa kubadilika sababu sioni cha kumzuia, mbona akialikwa kwenye
pati za rafiki zake huwa anakwenda lakini sehemu kama hizi haji?
Kilichotokea Airport ni funzo tosha, Mungu alimpa na akiendelea hivi
siku atakumbana na majanga mazito atakosa wa kumsaidia,” alisikika mmoja
wa wasanii waliokuwepo katika hafla hiyo.
Mara baada ya kupokea malalamiko hayo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka hivi:
“Sababu zangu kutohudhuria katika hafla zao wao wenyewe wanazijua na wakizijua wao inatosha siyo lazima nikwambie na wewe (mwandishi). Elewa tu hivyo.”
“Sababu zangu kutohudhuria katika hafla zao wao wenyewe wanazijua na wakizijua wao inatosha siyo lazima nikwambie na wewe (mwandishi). Elewa tu hivyo.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )