Miss
Ubungo 2014, Diana Joachim (kulia) akimkabidhi zawadi mtoto Anitha
Constantine ambaye anayeishi katika Kituo cha Chakuwama- Sinza.
Watoto wanaoishi kwenye kituo hicho cha kulelea yatima wakiwa katika picha.
Baadhi ya zawadi alizozitoa.
Baadhi ya zawadi alizozitoa.
MISS Ubungo 2014, Diana Joachim Kato,
jana aliwapa zawadi ya Pasaka ya vyakula na vinywaji watoto yatima wa
Kituo cha Kulelea Yatima ‘Chakuwama’ kilichopo Sinza jijini Dar es
Salaam.
Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa katibu
mtendaji wa kituo hicho, Hassan Hamis ambaye alimshukuru kwa msaada wake
kwa kuwakumbuka watoto yatima kusherehekea Sikukuu ya Pasaka pamoja
nao.
Mrembo huyo alisema kuwa lengo kubwa la
kwenda kutoa zawadi hizo ni namna alivyoguswa na moyo wake wa
kusherehekea Sikukuu ya Pasaka na watoto hao ikiwa ni kuwatia moyo ili
waweze kuishi katika maisha ya furaha.
“Nimeamua kuja kutoa zawadi hizi japo
kidogo lakini kwa Mungu ni kubwa hasa nikiangalia siku ya leo ni siku ya
furaha na kidogo nilichonacho nimependa niwape zawadi wafurahie sikukuu
hii,” alisema Diana.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )