Featured
Loading...

Necta Yapata Mwarobaini wa Udanganyifu Katika Udahili wa Wanafunzi Kwenye vyuo Ambayo Havijasajiliwa

Udanganyifu katika udahili wa wanafunzi kwenye vyuo ambayo havijasajiliwa kuanza kudhibitiwa, baada ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) kuzindua mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) kwa mwaka wa masomo 2016/17.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayuga na kusema mfumo huo utaanza kutumika kesho saa 6.00 mchana.

Dk Rutayuga amesema mfumo huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya astashahada, stashahada na shahada ya kwanza kwa kozi zote zinazotolewa na vyuo vikuu na taasisi zote za elimu nchini, tofauti na ilivyokuwa awali.

Amebainisha kuwa Serikali imeamua maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya ngazi hizo yafanywe kupitia mfumo huo.

Kaimu Katibu huyo alisema mfumo huo wa i utafanyika kwa utaratibu unaotambulika.

“Mfumo huu utatumika kudhibiti udanganyifu katika udahili na kugundua baadhi ya waombaji wanaotumia vyeti vya bandia,” amesema.

Amesema mfumo huo utaiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini na waombaji kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali peke yake.

Vilevile, Dk Rutayuga amesema mfumo wa CAS utawapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mtu mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja, hivyo kuwanyima wenzake nafasi.

Ofisa Mafunzo ya Kompyuta wa Necta, Daud Mabena amesema waombaji wanatakiwa kutembelea tovuti ya baraza ambayo ni www.nacte.go.tz na kufuata maelekezo ya udahili.

Gharama ya kutuma maombi kwa kozi moja ni Sh20,000 na zaidi ya moja Sh30,000.   

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top