Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia
Francis “SMG” Cheka kwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa
Super-Middle wa chama cha WBF baada ya kumtwanga kwa pointi bondia
Mserbia, Geard Ajetovic.
Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.
Akitoa
pongezi hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye alisema kuwa Rais amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao
umeipa heshima nchi katika medani ya michezo ndani na nje ya mipaka
yake.
Waziri
Nnauye alisema kuwa serikali imeweka utaratibu wa kuwapongeza
wanamichezo wanaofanya vyema kimataifa ili kuleta hamasa kwa wengine na
wale wanoafanya vizuri kuongeza bidii.
“Cheka
umefanya mambo makubwa sana, umeiletea sifa Tanzania na Rais
amefuraishwa sana, naomba kuongeza bidii na wengine kufuata nyayo zako,
nimefurahi kusikia kuwa mdogo wako, Cosmas naye ameshinda ubingwa wa
Afrika, nampongeza sana,” alisema Nnauye.
Katika
hafla hiyo, Serikali ilimpa cheti cha pongezi Francis Cheka na kumtaka
kuzidi kuitangaza nchi kupitia mchezo huo ambao ni wa kwanza katika
historia ya Tanzania kuleta heshima. “Serikali inaahidi kusaidia mchezo na mabondia ili kufikia maendeleo ya juu kabisa,” alisema.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Cheka aliipongeza serikali na kutambua mchango wake
katika kuleta sifa ya nchi hii na kuahidi kuleta mikanda mingi ya
ubingwa wa dunia.
“Nimefurahi kutambuliwa na serikali, nimepata hamasa kubwa sana, naahidi kufanya mambo makubwa katika mchezo huu,” alisema.
Mkurugenzi
wa Advanced Security, Juma Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka alisema
kuwa wamefarijika sana kupata pongezi za serikali na kuahidi kuandaa
mapambano mengi ya Cheka kwa mabondia wan je ya chi katika mapambano ya
ubingwa wa Dunia.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )