Akizungumza na kona ya Bongo Movies Shamsa alisema, hivi karibuni alienda saluni na kukutana na ujumbe wa Mkongo wa Wema, Wolper ukimuhitaji kimapenzi jambo ambalo lilimuudhi sana.
“Hii si mara ya kwanza kunitongoza kwani nakumbuka kuna siku mtu aliniomba namba ya simu na baadaye nikapigiwa na huyo Mkongo akinihitaji hotelini kuongea mambo ya filamu nikamwambia amtafute meneja wangu akakataa na kung’ang’ania niende mimi nikakataa,” alisema Shamsa.
Chanzo: GPL
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )